Johnson Minja.
Mwenyekiti wa wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja pichani juu amefutiwa kesi yake ya uchochezi iliyokuwa inamkabili katika mahakama ya
wilaya ya Dodoma.
Kwa
mujibu wa wakili wa Minja, Paul Malimi kesi hiyo ilifutwa Agosti 21
mwaka huu baada ya kuendeshwa kwa muda wa miezi nane tangu Januari 26
mwaka huu.
Malimi ametoa taarifa hiyo jana kwenye mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini uliofanyika mjini Dodoma.
Amesema mapema Agosti 21 aliitwa mahakamani na na kupewa hati ya
kufutwa kwa mashauri ya jinai yaliyokuwa yanamkabili mwenyekiti huyo wa
wafanyabiashara.
Amebainisha kuwa kesi hiyo imefutwa chini ya kifungu cha 91 (1) cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai sura ya 20.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania
(JWT), Johnson Minja amesema kuwa serikali itaweza kumkamata na
kumfungulia tena mashtaka kama ataendelea kuhamasisha wafanyabiashara
wasitumie mshine za kulipa kodi za EFDs kitu ambacho amesema kuwa hana
mpango wa kukifanya.
Amesema kuwa alijua kuwa atashinda kesi hiyo kwa kuwa hakufanya kosa.
Amesema kuwa hata kama kesi hiyo ingeendeshwa kwa miaka mingi zaidi
mbele alikuwa na uhakika wa kushinda kwa kuwa hakuwa na makosa.
Minja alikuwa anakabiliwa na makosa ya uchochezi, kwa kuwachochea
wafanyabiashara nchini kugomea kutumia mashine za kieletroniki
kukusanya kodi za EFDs hali iliyoisababishia taifa hasara ambayo
haikuwekwa wazi na mahakama.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment