August 20, 2015





Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini ametangaza rasmi kumsajili mchezaji wa Valencia ya La Liga , beki Nicolaus Otamendi leo Alhamisi kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 32.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina amefaulu katika vipimo vya afya na City na amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano na timu hiyo ya Barclays Premier League.
Otamendi amekuwa akihusishwa na kusajiliwa na vilabu vya Manchester United na  Real Madrid lakini amekuwa usajili wa tano wa Etihad baada ya kuwa tayari imewasaini wachezaji  Raheem Sterling, Fabian Delph, Enes Unal na Patrick Roberts.

Nicolaul Otamendi ni nani?
Anaitwa Nicolaus Hernan Gonzalo Otamendi, amezaliwa,Februari 12, 1988, Buenos Aires, Argentina, ana miaka 27 sasa, amecheza vilabu vya Porto ya Ureno, Atletico Mineiro ya Italia na Valencia ya Hispania. Akiwa amecheza jumla ya michezo 235 na kufunga magoli 18 kwa ngazi ya vilabu. H
uku akiwa na jezi ya Taifa ya Argentina amecheza michezo 25 na kufanikiwa kuifungia goli moja.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE