Sumaye anakuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa pili kujiunga na UKAWA baada ya Mhe.
Edward Lowassa kufanya hivyo.
Sumaye akiongea na vyombo vya habarileo mchana
Sumaye amejiunga rasmi na Ukawa wakati
wa mkutano wa wanahabari na viongozi wa Umoja huo, mkutano uliofanyika
mchana wa leo katika ukumbi wa hoteli ya Kunduchi jijini Dar.
Aidha Sumaye hakusema ni chama gani
amejiunga nacho, licha ya kubainisha lengo lake kuu la kuondoka CCM ni
kwenda kuimarisha Ukawa na kuongeza nguvu kwenye vyama vya upinzani hasa
katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment