August 13, 2015


Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kimetangaza majina ya wagombea ubunge, ubunge viti maalum, uwakilishi na uwakilishi viti maalum ambapo baadhi ya wagombea walioshinda kwenye kura za maoni wametupwa nje na kuchukuliwa mshindi wa tatu

Akizungumza leo na waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya CCM mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kuwa kuna baadhi ya majimbo ambayo yamelazimika kurudia kupiga kura za maoni na mengine kuhesabu upya kura zilizopigwa baada ya kujitokeza malalamiko kwa wagombea.

Amesema kuna baadhi ya majimbo ambayo wamelazimika kumchukua mshindi wa tatu kwenye kura za maoni na kuwaacha walioshinda nafasi ya kwanza na ya pili ili kumaliza migogoro iliyokuwepo.

Ameyataja majimbo 11 ambayo yatarudia uchaguzi wa kura za maoni kuwa ni Ukonga, Kiteto, Chilonwa, Kilolo, Njombe Kusini, Makete, Namtumbo, Rufiji, Mbinga Vijijini, Busega na Singida Mashariki.

Aidha Nnauye amesema kuwa uchaguzi wa viti maalum kupitia umoja wa wanawake Tanzania (UWT) yamepitishwa kama yalivyotoka mikoani ambapo ni mkoa mmoja tu wa Dar es Salaam ambao NEC imetengua ushindi wa mshindi wa kwanza, Angela Kiziga ambaye ni mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na badala yake aliyeshika nafasi ya pili na ya tatu ndiyo waliopitishwa katika ubunge wa viti maalum.

Waliopitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM kwenye ubunge wa viti maalum mkoa wa Dar es Salaam ni Mariam Kisangi aliyekuwa mshindi wa pili na Janeth Masaburi aliyekuwa mshindi wa tatu.

Related Posts:

  • Mbowe Anyang'anywa Gari Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kimesikitishwa na hatua ya uongozi wa Bunge la Tanzania ya kulichukua gari la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe alilokuwa akilitumia kwa sh… Read More
  • Watanzania hawatatuelewa - Mwakyembe   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amefunguka na kusema kuwa endapo watashindwa kufanya maandalizi mazuri ya michuano ya mataifa ya Africa (AFCON) kwa vijana 2019 basi Watanzani… Read More
  • Ancelotti atimuliwa Bayern   Kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti amefutwa kazi leo kufuatia mwanzo mgumu wa msimu wa 2017/18 yakiwemo matokeo ya jana usiku ambapo timu hiyo ilikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa PSG. Mkurugenzi … Read More
  • Daktari aeleza hatari ya vyuma vilivyoko kwenye moyo wa Manji   Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Aga Khan, Mustapha Bapumia (62) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anashangaa mtu mwenye umri mdogo kama Yusufali Manji (41) kuw… Read More
  • Mama yake Hayati Samuel Sitta Alipoikaribisha Tigo Fiesta Tabora   Kama ilivyo kawaida ya FIESTA, huambatana na matukio mbalimbali ya Kitaifa, Kwa mkoa wa Tabpora watasherehekea Fiesta siku ya Ijumaa 01 Oct .Geah Habib alipata nafasi ya kutembelea nyumbani kwa Hayati Spika wa B… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE