August 14, 2015

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Kala Jeremiah akiongea na waandishi wa habari ili kuwaelezea ...

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Kala Jeremiah akiongea na waandishi wa habari ili kuwaelezea onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. Pembeni ni Joseph Haule “Professa J”, Juma Kassim “Sir Nature” pamoja na Msagasumu.

 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. 

 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Juma Kassim “Sir Nature” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.

Tanzania Oyeeeee! Tanzania Oyeeee! ndiyo wasanii hawa walivyokuwa wakitia msisitizo.

 Baadhi ya wasanii watakaowasha moto Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.

Mwandishi wa habari wa Times Fm, akifanya mahojiano na Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J”.
--

Na Mwandishi Wetu.

Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya na baadhi ya nyota wa Bongo Movie watafanya onyesho la bure Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.

Wasanii hao wataongozwa na Mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi “Sugu” na nyota wengine kama Juma Kassim “Sir Nature”, Joseph Haule “Professa J” na Kara Jeremiah.

Wengine ni watakaopanda jukwaani siku kuanzia saa 8.00 mchana ni Msaga Sumu, Baba Haji na waigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper na Auntie Ezekiel.

Akizungumza jijini jana, Professa J alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya onyesho hilo ni kutoa elimu kwa mashabiki wao kuhusiana na zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi bora wan chi hii wataodumu kwa miaka mitano.

Professa alisema kuwa wanataka kutoa mwamko kwa mashabiki wao kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo ili kutumia demokrasia yao kumchagua kiongozi wanayemtaka.

“Tumejiandaa vilivyo kutoa elimu, lengo ni kuwahamasisha mashabiki wetu kufanya kile wanachokiona kinafaa ili kutimiza malengo yao ya kikatiba,” alisema Professa J.

Alisema kuwa mbali ya Dar es Salaam, onyesho hilo pia litafanyika katika mikoa mengine mbalimbali.

Akizungumza katika mkutano huo, Nature aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kupata elimu hiyo ambayo wasanii wameamua kuitoa.

“Hii siyo kampeni ya kisiasa, sisi ni wasanii tumeamua kujitolea kufanya kazi ambayo wasanii wengi duniani wameifanya, lazima tutumie kazi yetu kutoa elimu kwa mashabiki ili wajue wajibu wao katika mambo mbali mbali pamoja na uchaguzi mkuu,” alisema Nature

Related Posts:

  • MAFANIKIO YA CHAMELEONE KATIKA MAISHA . Baada ya kukutana na staa wa muziki kutoka Uganda Jose Chameleone nimegundua kuna mambo mengi nilikua nayasikia tofauti na kuyasoma ambayo yeye ameyazungumza tofauti kabisa. Nilikua sijui, kumbe Chameleo… Read More
  • HIVI NDIVYO SINGLE BOY YA KIBA ILIVYOKUWA Ni miongoni mwa vipande vya video ya single boy Ally Kiba                   Diamond Mwanzoni mwa mwezi march au mwishoni mwa m… Read More
  • WEWE MKAZI WA MOROGORO SAS BHAAAS NI USIKU  WA   JUMAA  TANO YA  TAREHE  18  JULY 2012, NDANI  YA  4 STAR  SELENGETI   FIESTA  SUPA  NYOTA KUUDONDOSHA  MZIG O MZIMA  NDANI  … Read More
  • AFANDE SELE AMFUNGUKIA 20% Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!! Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twent Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award. "Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabl… Read More
  • P SQUARE WAPATA PIGO. Mrs. Okoye Mrs. Okoye amekuwa akiumwa kwa mrefu ugonjwa ambao bado haujajulikana. Pamoja na Peter na Paul, watoto wake wengine  Jude na Ajeh  wana mchango mkubwa kwenye muziki wa Nigeria. Pe… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE