Ziito Kabwe akiwa na mume wa Chiku Abwao na Chiku Abwao na kada wa ACT wazalendo.
Zitto kabwe akiwa na wapambanaji
Zitto kabwe akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini
Chiku Abwao akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini
Mgombe udiwani wa kata ya Mvinjeni Abuu Majeck akimpongeza mgombea ubunge jimbo la Iri nga mjini Chiku Abwao
KIONGOZI wa chama cha ACT Wazalendo amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kuwa ni miongoni mwa wabunge wa mfano kutokana na utendaji kazi wake mkubwa badala ya maneno bila vitendo.
Huku aliyekuwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao akimtaka mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (chadema) kuwaeleza wakazi wa jimbo hilo ndani ya miaka mitano ya ubunge wake amefanya nini zaidi ya maandamano na kutukana watu .
Kauli hiyo waliotoa wakati wa mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha wagombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini na majimbo mengine ya mkoa wa Iringa na kuwa siasa si maneno matupu siasa ni kazi zaidi ya kuwakomboa wananchi waliokuamini katika maendeleo .
Alisema Bw Kabwe kuwa mbali ya kuwa yeye ni ACT wazalendo ila hata acha kuwazungumzia baadhi ya wabunge waliofanya kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi wao na miongoni mwa wabunge hao ni pamoja na mbunge wa Ludewa Bw Filikunjombe kwani kazi aliyoifanya jimboni inaonekana na kazi aliyoifanya ndani ya bunge katika kupigania maendeleo ya wana Ludewa na Taifa kila mtazania anatambua mchango wake .
Kwani alisema kuwa kati ya manho makubwa ambayo Filikunjombe kama makamu wake mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kamati liyoifanya ni pamoja na kuhakikisha ripoti ya Escrow inalindwa pasipo kuibiwa wakiwa wabunge watatu ambao walikesha wakilinda ripoti hiyo isiibwe na mawaziri waliokuwa wakizingira jengo walilokuwepo ili kuiba ripoti hiyo .
'' Siku ile tulikesha na mashuka yetu ya kimasai kuhakikisha ripoti yetu haiibwi ili tuiingize bungeni na tukaiingiza bunge lakini ile ripoti hadi leo kuna mambo hayajamalizwa kwani kampuni ya IPTL ambao imenunuliwa na kampuni ya PAP ya Singa singa na kampuni hiyo ya PAP hadi leo bado inapokea Tsh bilioni 4 kila mwezi kutoka Tanesco hapo wazalishe ama wasizalishe'' alisema Kabwe
Alisema kuwa kampuni hiyo asilimia 50 inamilikiwa na Seth Singa singa na asilimia 50 nyingine zinamilikiwa na kampuni inaitwa simba Trust iliyosajiliwa nje ya Tanzania na wamiliki wake hawafahamiki na kuwa hizo ndizo hoja ambazo ACT wazalendo wamejiandaa kutembea nazo katika kampeni ya uchaguzi mkuu .
Kabwe alisema kuwa sakata ya ECROW bado halijaisha kwani bunge liliagiza mtambo wa IPTL utaifishwe ila hadi leo bado kuna kigugumizi katika kuchukua hatua juu ya suala hilo la kampuni ya kitapeli kuendelea kulipwa mabilioni ya shilingi hivyo alisema kuwa haja ya chama cha kati kuingia Ikulu ili kuweza kupambana na mafisadi wa Richimond ambao leo wamejificha katika mwamvuli wa UKAWA .
Hivyo alisema kuwa kila sababu wabunge kufanya kazi wanayotumwa na wananchi wao kwa uadilifu badala ya kuwa wabunge wa maneno bila vitendo na kuwa wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu ni vema wananchi kuwapima wabunge wanaowachagua kwa kueleza wamefanya nini majimboni badala ya kuwa na mbunge mpiga kelele zisizo za kimaendeleo kwa wananchi wake .
Kwa upande wake mgombea ubunge wa ACT wazalendo jimbo la Iringa mjini Bi Abwao ambae amejiunga na chama hicho kutoka Chadema alisema mbunge wa jimbo hilo mchungaji Msigwa ajiandae kukabidhi jimbo hilo kwa ACT wazalendo kwani ameshindwa kuwatumikia wananchi wa jimbo la Iringa mjini kazi waliyomtuma bungeni .
Alisema kuwa kipindi cha miaka mitano ya mbunge mchungaji Msigwa jimboni hapo hakuna jipya ambalo amelifanya zaidi ya maandamano na vurugu ambazo wakazi wa Iringa mjini hawajapata kuziona na kuwa atazunguka kila moja hadi nyingine kuwaeleza wananchi jinsi ambavyo mbunge huyo alivyojaribu kuua nguvu ya vyama vya upinzani na kushindwa kuwajibika kwa wananchi waliomchagua
August 10, 2015
6:34 AM
Machaku
No comments
Related Posts:
NMB yawashukia wafanya biashara wadogo kuwakwamua kiuchumi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa NMB FANIKIWA ACCOUNT uliofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaa… Read More
Diamond amepost hivi baada ya kifo cha mume mwenzie Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond Platnumz ameandika ujumbe huu "Mbele yako, Nyuma yetu" Ujumbe huo ni baada ya Aliyekuwa mume wa Zarina Hassan ‘Zari The Bosslady’, Ivan Semwanga kufariki dunia akiwa hospitali… Read More
Brand New Video: Lavalava - Tuachane Kutoka WCB, wanakuletea Video ya msanii wao mpya kabisa anayefahamika kwa jina la Lavalava wanakuletea Video ya wimbo wa msanii huyo uitwao Tuachane. Bofya hapa chini kutazama … Read More
Kisa Mahojiano ya RC Makonda..Mtangazaji Cyprian Musiba wa Radio Free Africa Aamua Kuacha Kazi Mtangazi na kiongozi wa Radio Free Africa bwana Cyprian Musiba ameamua kuacha kazi kutokana na issue ya maadili mara baada ya mahojiano ya Rc Makonda. Kupitia ukurasa wake wa insta amebainisha hayo. … Read More
Breaking News:Mzazi mwenzie na Zari The boss Lady amefariki Dunia Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema mzazi mwenzie na Mfanya Biashara maarufu Zari The boss Lady anayefahamika kwa jina la Ivan Semwanga a.k.a Ivan the Don, mfanyabiashara maarufu nchini Uga… Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment