Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Saudi Arabia inabeba dhima
ya ajali ya hivi karibuni ya winchi au kreni katika Masjidul Haram Makka
ambapo mahujaji zaidi ya 107 walipoteza maisha.
Hussein Amir Abdulahian, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema
uzembe wa wakuu wa Saudi Arabia na kutozingatiwa kanuni za usalama ndio
chanzo kikuu cha ajali ya Makka ambayo pia lilipelekea zaidi ya watu 230
kujeruhiwa. Uchunguzi kuhusu ajali hiyo ya Ijumaa iliyopita Makka
umebaini kuwa kulikuwa na kosa la kiufundi katika winchi iliyowaangukia
mahujaji na wala si upepo mkali kama ilivyodaiwa. Shirika la Binladin
lenye kandarasi ya kupanua Masjidul Haram limelaumiwa kwa kutozingatia
sheria za ujenzi katika kazi zake. Huku hayo yakijiri, Alkhamisi ya jana
kuliibuka moto mkubwa katika hoteli moja ya mahujaji mjini Makka ambao
watu wawili walijeruhiwa huku watu wote zaidi ya 1000 waliokuwa ndani ya
hoteli hiyo wakiondolewa mara moja ili kuepusha maafa.
September 18, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment