Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu akifafanua jambo
Wamiliki wa mitandao ya mawasiliano nchini wametakiwa kutoa taarifa
haraka juu ya makosa ya uharifu wa mitandaoni pindi yanapojitokeza, ili
kuvirahisishia vyombo vya usalama kuweza kuchukua hatua za haraka kwa
wahusika.
Wito
huo umetolewa leo mkoani Mtwara na mkuu wa upelelezi wa polisi wilaya
ya Masasi, SP Nathaniel Kyando, wakati wa semina ya mahakimu, waendesha
mashitaka na wapelelezi kuhusu elimu ya sheria ya makosa ya mtandao na
sheria ya miamala ya kielektroniki ya mwaka 2015.
Kwa upande wake, mkuu wa kitengo cha sheria kutoka Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Veronica Sudayi, akizungumza kwa
niaba ya katibu mkuu wa wizara hiyo, amesema jamii inatakiwa kufahamu
kwamba sheria hiyo haina vitu vipya isipokuwa ni mabadiliko ya kimfumo
ambayo yameingiza makosa hayo katika mfumo wa kielektroniki.
Aidha, mwanasheria kutoka wizara hiyo, Anna Kalamo, amesema miongoni
mwa mada ambazo wanapatiwa wahusika ni pamoja na sheria mbili ambazo
zimepitishwa na serikali za miamala ya kielektroniki na sheria ya makosa
ya mitandao zote za mwaka 2015 ambazo zimetungwa kwa lengo la kuleta
ulinzi na matumizi salama ya mitandao hapa nchini.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment