November 21, 2015

Chama cha ACT -Wazalendo kimetoa taarifa kuhusu  Kubaki Bungeni kwa mbunge wake wa Kigoma mjini Ndugu Zitto Zuberi kabwe na kusema ulikuwa ni msimamo wa chama. Kitila mkumbo katibu Mkuu wa ACT ameeleza kupitia ukurasa wake wa Facebook
"Ieleweke tu kuwa alichokifanya Zitto bungeni jana ni msimamo wa Chama chetu cha ACT Wazalendo. Tunaamini kwamba matatizo ya Zanzibar yatatatuliwa kwa njia za kisheria na kisiasa. Na tusingeweza kushiriki kutekeleza mpango ambao hatukushiriki kuupanga. Sisi pia tunamtambua DK Magufuli kama mshindi halali wa kiti cha urais na Mgombea wetu alikubali matokeo. Sisi sio mazuzu au nyumbu hata tujiegeshe katika mipango tusioijua. We're a political party with a clear set of principles, values and mode of operations.
Tutaendelea kushirikiana pale ambapo hoja zinashabihiana. Lakini pia hatutaogopa kutofautiana pale ambapo hatuamini katika msingi wa hoja au njia za utekelezaji. Katika hili la Zanzibar tunafanana katika msingi wa hoja lakini tunatofautiana katika mkakati wa utekelezaji wa hoja husika. Na hii haina ubaya wowote, ni afya kabisa kwa demokrasia yetu. Kuwaita watu mnaotofautiana mitazamo kwamba ni wasaliti ni kielelezo kamili cha ujinga wa kisiasa. Na Sisi tumedhamiria kupambana na ujinga wa kisiasa popote ulipo"
Kitila Mkumbo
Mshauri wa Chama

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE