November 21, 2015


Mh: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amelifungua bunge la 11 kupitia hotuba yake ya jana bungeni iliyojaa kila aina ya ushawishi wa kuwalejesha watanzania katika matumaini mapya. Hotuba ilijaa uzalemdo, uchungu wa nchi na mahaba tele kwa taifa letu.
  
Hapa Mh: Julius Mtatiro anafunguka kuhusu Hotuba hiyo ya Mh: Rais
"Ukimsikiliza John Pombe Magufuli, unaweza kudhani kuwa kabla yake hakukuwa na serikali iliyokuwa inaongozwa na chama chake na viongozi wenzake.
Mambo yote anayoongea ni yale yale ambayo marais wenzake Mwinyi, Mkapa na baadaye Kikwete waliyaahidi kwa msisitizo mkubwa lakini baada ya miaka mitano au Kumi hali ya wananchi, wafanyakazi, wakulima na sekta za nchi zilizidi kuwa hoi bin taabani.
Naikumbuka sana ahadi ya Kikwete tangu 2005 na 2010 juu ya kupunguza matumizi ya anasa na yasiyo na lazima, lakini leo JPM anatueleza kuwa serikali ya Kikwete bila kuhusisha takwimu za taasisi ya Rais, katika mwaka wa fedha 2013/14 na 2014/15 imetumia zaidi ya bilioni 300 za Tanzania kwa ajili ya safari za nje ya nchi huku kati ya pesa hizo zaidi ya bilioni 180 zikitumika kununua tiketi za ndege.
Takwimu nyingine (zisizo rasmi sana) zinaonesha kuwa serikali ya Kikwete kwa miaka 10 imetumia karibia shilingi trilioni 2 (bilioni 2000) kwa ajili ya safari za nje, fedha hizi zingeliweza kujenga kilomita 2500 za lami.
Hiyo ina maana kuwa Kikwete na wenzake walikuwa ni "kikundi cha matumizi na matanuzi". Hapa sijaongelea "mikwara" iliyowahi kupigwa na Mwinyi na Mkapa huko nyuma na haikutekelezeka hadi leo.
Hii inaashiria kwamba mabadiliko yanayohitajika Tanzania ni zaidi ya mabadiliko ya mtu mmoja au wawili, ni mabadiliko ya mfumo wote na kuweka mfumo mpya.
Wakati watu wanaamini kuwa tumepata mwarobaini wa matatizo na kero za nchi yetu, mimi bado nasema baada ya miaka mitano wengi wenu mtakuwa mkiilalamikia sana serikali hii inayoundwa na chama kilekile chini ya mfumo uleule.
NOTE; Siku hazigandi, tuchangie huku tunaweka akiba ya maneno. POST hii ntai-repost tena mwezi Disemba 2019.
Mtatiro J.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE