November 01, 2015


Kaya 30 za kata ya Kilakala manispaa ya Morogoro hazina makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa maji kufuatia mvua zilizo nyesha mda mfupi na kusababisha maji kuacha muelekeo baada ya kuziba mifereji ya kuyapitisha kisha kuingia katika makazi ya wananchi.

Wakizungumza kwa masikitiko wananchi hao wametupia lawama serikali kushindwa kuwasimamia watengeneza barabara ambao wamesababisha kujaa michanga katika mifereji kisha maji kukosa muelekeo na kujaa katika makazi ya watu.

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Kilakala Gabrieli Maurus pamoja na diwani mteule wa kata hiyo Mabulla Rashidi wamesema serikali inatakiwa kuto wafumbia macho wakandarasi ambao wanapewa kazi na kutomaliza kwa wakati ilikuepuka usumbufu na kero kwa wananchi

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE