
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufuatia taarifa iliyotolewa na
Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kikao cha Kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyokutana Zanzibar juzi,
tarehe 27 Desemba, 2015, waandishi wengi wa habari wametupigia simu
wakitaka kujua Chama Cha Wananchi (CUF) kimepokea vipi taarifa ile.
Vikao vya CCM ni vikao vya CCM. Si kawaida yetu kutolea taarifa maamuzi ya vikao vya vyama vyengine. Hata hivyo, tunaelewa ni kwa nini kumekuwepo na shauku ya kusikia CUF inasema nini kwa sababu yale yaliyokuwemo kwenye taarifa hiyo yaligusia pia mazungumzo yanayofanyika Ikulu Zanzibar yanayolenga kupata ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.
Vikao vya CCM ni vikao vya CCM. Si kawaida yetu kutolea taarifa maamuzi ya vikao vya vyama vyengine. Hata hivyo, tunaelewa ni kwa nini kumekuwepo na shauku ya kusikia CUF inasema nini kwa sababu yale yaliyokuwemo kwenye taarifa hiyo yaligusia pia mazungumzo yanayofanyika Ikulu Zanzibar yanayolenga kupata ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.
Baada ya kuipitia taarifa ya
CCM na mengine yaliyoelezwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Zanzibar wakati akitoa ufafanuzi wa yale yaliyomo kwenye taarifa hiyo,
CUF tunapenda kuwaeleza Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla haya
yafuatayo:

1. Taarifa yenyewe haionekani kama imeandaliwa na watu
makini wala haioneshi kama walioitoa wanajua nini kilichopo. Hilo liko
wazi kutokana na taarifa yenyewe kuwa na maudhui yanayopingana ambayo
yamekuja kukorogwa zaidi na maelezo yaliyotolewa na Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM Zanzibar mbele ya waandishi wa habari na kuoneshwa katika
vituo kadhaa vya televisheni:
(a) Taarifa inawataka wanachama wa
CCM wajiandae na uchaguzi wa marudio lakini papo hapo inaeleza kwamba
kikao kimeridhia mazungumzo yanayoendelea Ikulu Zanzibar. Taarifa
haisemi iwapo maamuzi ya vikao vya mazungumzo hayatakuwa na suala la
kurudiwa uchaguzi, upi ni mwelekeo wa CCM.
(b) Taarifa inazungumzia uchaguzi wa marudio lakini papo hapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar anasema CCM haina imani na Tume ya Uchaguzi iliyopo na kwa hivyo uchaguzi huo wa marudio lazima ufanyike chini ya Tume mpya. Baada ya hapo hasemi Tume iliyopo ambayo muda wa utumishi wa Makamishna wake unalindwa kikatiba itaondolewa vipi na Tume mpya itapatikana vipi.
(c) Taarifa inawataka wanachama wa CCM wajiandae na uchaguzi wa marudio lakini Katibu wa itikadi na Uenezi anasema hata usiporudiwa ndani ya siku 90, bado Dk. Ali Mohamed Shein ataendelea kuwa Rais.
Nukta hizi tatu ambazo haziwezi zote kusimama kwa pamoja bila ya kupingana moja dhidi ya nyengine zinaonesha tu ni kwa kiasi gani viongozi wa CCM Zanzibar wamepoteza mwelekeo na hawana uhakika wa nini kitatokea katika kuondokana na mgogoro huu wa kutengenezwa.
(b) Taarifa inazungumzia uchaguzi wa marudio lakini papo hapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar anasema CCM haina imani na Tume ya Uchaguzi iliyopo na kwa hivyo uchaguzi huo wa marudio lazima ufanyike chini ya Tume mpya. Baada ya hapo hasemi Tume iliyopo ambayo muda wa utumishi wa Makamishna wake unalindwa kikatiba itaondolewa vipi na Tume mpya itapatikana vipi.
(c) Taarifa inawataka wanachama wa CCM wajiandae na uchaguzi wa marudio lakini Katibu wa itikadi na Uenezi anasema hata usiporudiwa ndani ya siku 90, bado Dk. Ali Mohamed Shein ataendelea kuwa Rais.
Nukta hizi tatu ambazo haziwezi zote kusimama kwa pamoja bila ya kupingana moja dhidi ya nyengine zinaonesha tu ni kwa kiasi gani viongozi wa CCM Zanzibar wamepoteza mwelekeo na hawana uhakika wa nini kitatokea katika kuondokana na mgogoro huu wa kutengenezwa.
2. Taarifa ya CCM
haiwasaidii wanachama wa CCM wala wananchi wa Zanzibar kwa kuwapa
matumaini ya kumalizika kwa mgogoro wa kutengenezwa wa uchaguzi wa
Zanzibar na badala yake inaonekana imelenga kuwachanganya zaidi wananchi
kwa maelezo yanayopingana.
3. Taarifa inaonyesha ni jinsi gani
CCM kilivyopoteza mvuto kwa kujiweka mbali na wananchi. Taarifa hiyo
inapongeza eti kuwepo kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii wakati
wananchi wa Zanzibar, bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, siyo tu
wanumia kutokana na sera mbovu za CCM lakini sasa wanazidi kuteketea na
maisha yao kuwa magumu zaidi kutokana na fadhaa (tension) na taharuki
iliyopo katika nchi kutokana na kutokuwepo kwa Serikali yenye ridhaa
yao. Harakati za maisha zimeathirika sana huku bidhaa vikiwemo vyakula
vikipanda bei. Viongozi wa CCM hawaonekani kujali hali hii mradi wao yao
yanawaendea. Tabia hii ya CCM kutowajali wananchi wanyonge wa nchi hii
ndiyo iliyopelekea wananchi kukiadhibu chama hicho katika uchaguzi mkuu
na kupelekea mgombea wake wa Urais wa Zanzibar na wagombea Uwakilishi
kushindwa vibaya kwa tofauti ya zaidi ya kura 25,831.
4. Taarifa
inaendeleza utamaduni wa unafiki wa kisiasa kwa eti kuwapongeza viongozi
wa CCM na jumuiya zake kwa kazi ya kukiimarisha chama chao huku wakijua
kwamba viongozi wao hasa wale walioongoza Kamati ya Kitaifa ya Kampeni
za CCM Zanzibar walishindwa kazi na kupoteza mwelekeo. Matokeo ya kazi
mbovu ya Kamati ya Kampeni ya CCM Zanzibar ni kukisababishia chama hicho
kipigo kikubwa katika uchaguzi huo kilichopelekea kushindwa katika
nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa zaidi ya kura 25,831 na kupoteza viti
tisa (9) vya Uwakilishi kisiwani Unguja mbali ya kutopata hata kiti
kimoja kisiwani Pemba. Viongozi hao walishindwa kuwajibika licha ya
kutumia mabilioni ya fedha walizopewa kwa ajili ya kampeni.
5.
Katika maelezo yake ya ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar anaitupia lawama Tume nzima ya
Uchaguzi ya Zanzibar kwa kushindwa kazi huku akijua na ikijulikana na
kila mmoja kwamba tamko la kufuta uchaguzi limetolewa na Jecha Salim
Jecha kinyume na Katiba, kinyume na Sheria ya Uchaguzi na kinyume na
maadili ya kazi yake. Katiba inataka Jecha achukuliwe hatua za kufukuzwa
kazi kwa kuanza na kumuundia Tume Maalum ya kumchunguza, na siyo
kutafuta mbinu za kumlinda kwa kuwaingiza wasiokuwemo.
6. Maelezo
ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar kwamba Dk. Ali Mohamed
Shein ataendelea kuwa Rais hata baada ya miezi mitatu ni kielelezo na
ushahidi mwengine wa jinsi CCM isivyoheshimu Katiba. Kwa hakika, hili
suala la kutaja siku 90 ambalo linatajwa sana na CCM na wapambe wake
haijulikani hata linatokea wapi. Hakuna pahala popote katika Katiba ya
Zanzibar wala Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar panapotajwa sharti la
kurudiwa uchaguzi ndani ya siku 90 kwa sababu Katiba yenyewe na Sheria
ya Uchaguzi haina sehemu yoyote inayozungumzia kufuta uchaguzi na
kufanya uchaguzi wa marudio.
7. Kwa ujumla, taarifa ya CCM
Zanzibar iliyotolewa na Katibu wake wa itikadi na Uenezi inaonyesha
jinsi chama hicho kisivyojali madhila wanayoyapata raia, fedheha
iliyopata taifa na hali ya kiuchumi inayozidi kudorora kila siku
Zanzibar ikiwaathiri mno wananchi wanyonge.
Baada ya uchambuzi huo wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, CUF inapenda kuwaeleza Wazanzibari yafuatayo:
1. Waipuuze taarifa hiyo ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar
kwani haina lolote jipya zaidi ya kutaka kufunika kombe kutokana na
hali ngumu inayotokana na hoja za viongozi wa ngazi za chini na
wanachama wa CCM wanaotaka maelezo ya kwa nini chama hicho licha ya
kutumia mabilioni ya shilingi kimeshindwa vibaya katika uchaguzi mkuu.
2. Wazanzibari wasubiri taarifa rasmi ya matokeo ya mazungumzo
yanayowahusisha viongozi wakuu wa kisiasa yanayofanyika Ikulu Zanzibar
ambayo yamo katika hatua za mwisho kumalizika.
3. Wampe nafasi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli,
ambaye anaendelea na juhudi katika ngazi za juu kabisa za kuhimiza
kupatikana ufumbuzi wa haraka wa mgogoro wa uchaguzi wa tarehe 25
Oktoba, 2015.
4. CUF inawahakikishia Wazanzibari kwamba
haitotetereka na itasimamia kwa dhati maamuzi yao waliyoyafanya kwa njia
za kidemokrasia kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na
italinda chaguo lao la Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani wao.
5. Mwisho kabisa, inaendelea kuwapongeza Wazanzibari kwa kuonesha
ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa na kuendelea kutunza amani na utulivu
wakati wakisubiri matokeo ya kazi kubwa waliyoifanya tarehe 25 Oktoba,
2015 ambayo inaashiria ujenzi wa Zanzibar Mpya.
HAKI SAWA KWA Cuf Neema Kwa Wote
ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO NA UMMA – CUF
29 DESEMBA, 2015
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO NA UMMA – CUF
29 DESEMBA, 2015
0 MAONI YAKO:
Post a Comment