December 12, 2015

Gambia 

Rais wa Gambia Yahya Jammeh ametangaza taifa hilo lenye Waislamu wengi kuwa jamhuri ya Kiislamu, hatua ambayo anasema inakatiza kabisa uhusiano na historia ya zamani ya kikoloni.
Bw Jammeh ameambia runinga ya taifa kwamba tangazo lake linaambatana na sifa na maadili ya kidini ya Gambia.
Ameongeza kuwa raia na wageni wa dini nyingine hawatalazimishwa kuvalia mavazi ya Kiislamu, na wataruhusiwa kuendelea na dini zao bila kusumbuliwa.
Asilimia 90 ya raia wa Gambia ni Waislamu.
Koloni hiyo ya zamani ya Uingereza hutegemea sana utalii. Uhusiano kati ya taifa hilo na nchi za Magharibi umekuwa ukidorora siku za karibuni.
Muungano wa Ulaya ulikatiza kwa muda pesa za msaada kwa Gambia mwaka jana kutokana na rekodi mbaya ya haki za kibinadamu.
Bw Jammeh ameongoza taifa hilo ndogo la Afrika Magharibi kwa miaka 21.
Mataifa mengine yanayojitambulisha kama jamhuri za Kiislamu ni Iran na Pakistan, na barani Afrika kuna Mauritania.
Bw Jammeh aliondoa Gambia kutoka kwa Jumuiya ya Madola 2013 akitaja muungano humo kuwa wa ukoloni mamboleo.
Mwaka 2007, alidai kuwa alikuwa amepata dawa ya kiasili ambayo ingetibu Ukimwi.

Related Posts:

  • KUNDI LA BLUE 3 KURUDI TENA UPYAA..!! Ex Blu3 star who is now rumoured to be back to the group after they reunited with Jackie and Lillian has shown the other side of her by coming to the rescue of a one year old who was burnt by her father after a simple… Read More
  • .SHILOLE AINASA, MWENYEWE ATHIBITISHA KATIKA hali isiyo ya kawaida msanii wa filamu na muziki bongo, Shilole, ametangaza kuwa na ujauzito kitu ambacho anaamini kwa kufanya hivyo atapata baraka kutoka kwa mashabiki wake. Mwandishi wa habari hizi … Read More
  • SELE CHID BEENZ BIFU ZITO    Msanii Afande Sele aligeuka mbogo baada kumjibu msanii mwenzake Chid beenz kuwa hawezi kumteka na hana uwezo huo kwani Afande ameshakua mwanajeshi JWTZ na akaacha jeshi hivyo awezi kutishiwa amani n… Read More
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - TAMASHA LA MICHEZO TAMASHA LA MICHEZO LILILOANDALIWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA KUSHIRIKIANA NA UBALOZI WA SERIKALI YA UINGEREZA NCHINI KUPITIA SHIRIKA LA ‘BRITISH COUNCIL’ TAREHE: 27, MACHI, 2012MUDA: 4 Asb- 7… Read More
  • JOBFIRE A.K.A (SAUTI ZA MATUKIO) ASAKA MDHAMINIPICHANI NI MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA ANAYEJULIKANA KWA JINA LA JOBFIRE A.K.A SAUTI ZA MATUKIO,, NI MZALIWA WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO ILA KAZI ZAKE KIMUZIKI ANAFANYIA KISIWANI ZANZIBAR, CHIMBUKO LAKE NI MKOA WA TANGA,… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE