Baadhi ya wanawake wa manispaa ya Songea mkoani hapa wamedai kuwa ndoa nyingi zina migogoro na hazidumu kwa sababu wanaume wanakuwa na wapenzi wengi hali inayosababisha kushindwa kumudu kutimiza mahitaji ya familia zao.
Wakizungumza kwenye kongamano la haki za binadamu lililofanyika katika kijiji cha Sanangula manispaa ya Songea wanawake hao wamedai wanaume wenye wake na wapenzi wengi ndoa zao zinayumba kwa sababu wake zao wanakosa haki ya msingi ya ndoa jambo linalowafanya wanawake hao washindwe kuvumilia.
Sister Antony wa shirika la mabinti wa Maria Imakulatha kutoka nchini India (DMI) Jimbo la Songea amesema shirika hilo limewawezesha wanawake kwa kuwapatia mikopo midogo midogo fedha na pembejeo za kilimo kwa riba ndogo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment