Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mama Anna Mghwira amesema endapo serikali
ingeelekeza nguvu zake kwenye uzoaji taka, zingeweza kuongeza ajira kwa
kutengenezwa viwanda ambavyo vitatumia taka hizo katika uzalishaji wa
bidhaa
Akizungumza
na East africa Radio Mama Anna amesema kuwa kwa nchi nyingine taka ni
mali ambapo zinaweza kutengeneza viwanda zaidi ya vitatu ambavyo
vinaweza kutoa ajira na kukuza uchumi wa nchi.
Mama Anna ameongeza kuwa endapo fedha zilizotengwa kwa ajili ya
shughuli ya Uhuru zingetumika katika uwekezaji wa takataka hizo ikiwemo
kutengeneza madampo makubwa ya kuhifadhia taka hizo ambazo zinaweza
kutumika katika shughuli tofauti za kuliingizia taifa kipato.
Mwenyekiti huyo wa ACT amesema takataka hizo zinaweza kutengeneza
viwanda vya chuma, chupa, mbolea, karatasi ambapo wajasiriamali wanaweza
kupata fursa ya kuwekeza katika maeneo hayo.
Aidha amesema tatizo la uchafu katika majiji nchini kubwa ambapo
unahitajika mpango maalum wa kuweza kuyasafisha ili kuitoa Tanzania
kutoka katika nchi yenye majiji machafu kuelekea kwenye hali ya wastani
ya usafi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment