December 18, 2015

Kagame 

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametetea uamuzi wa taifa hilo kuandaa kura ya maoni kuhusu muhula wa rais akisema lilikuwa wazo la Wanyarwanda.
Raia nchini humo wamepiga kura leo kuhusu marekebisho ya katiba ambayo huenda yakamuwezesha Bw Kagame kutawala hadi 2034.
Alipoulizwa na mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga kuhusu wazo la kubadilisha katiba, Bw Kagame alijibu: “Sikuomba hili lifanywe, nenda kawaulize Wanyarwanda mbona wakajiingiza katika hili.”
Bw Kagame hata hivyo alisema ukiangalia rekodi yake uongozini “labda unaweza kupata wazo na kujua ni yapi yanatarajiwa.”
Kiongozi huyo bado hajatangaza iwapo atawania tena baada ya muhula wake kumalizika 2017, na amesisitiza kwamba atatangaza hilo baada ya kura ya maoni.
Lakini kuhusu mipango yake ya siku za usoni kuhusu Rwanda amesema: “Wana (Wanyarwanda) mustakabali gani? Si mimi ninayedhibiti mustakabali wao. Wanashikilia hatima yao mikononi.”
Bw Kagame alipiga kura katika kituo cha Rugunga mjini Kigali.
Wapiga kura walikuwa wakipigia marekebisho ya katiba ya 2015, na miongoni mwa mengine kupunguza muda wa rais kuhudumu kuwa mihula miwili ya miaka mitano badala ya saba.
Kagame 
 
Hata hivyo kutakuwa na kipindi cha mpito cha miaka saba kuanzia 2017 na Bw Kagame anaruhusiwa kuwania.
Hii ina maana kwamba anaweza kuongoza kwa miaka saba kuanzia 2017 kisha aongoze mihula miwili ya miaka mitano mitano, hadi 2034.
Kipindi cha maseneta kuhudumu pia kitaongezwa kutoka muhula mmoja wa miaka minane hadi mihula miwili ya miaka mitano mitano.
Mahakama za Gacaca, zilizoendesha kesi dhidi ya watuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya 1994 pia zitavunjwa.
Mahakama hizo zimemaliza kazi baada ya kusikiza kesi dhidi ya watu 2 milioni.

Related Posts:

  • Picha: Wakazi wa Kibamba Wauzuia Msafara wa Makonda Wakidai Kudhulumiwa Ardhi Wakazi wa Kibamba Wilayani Ubungo wamezuia msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonesha kuwa wamedhulumiwa ardhi yao.Mapema leo mchana mkuu huyo wa mkoa alitembelea mradi… Read More
  • Fidel Castro afariki dunia akiwa na miaka 90   Fidel Castro, kiongozi wa zamani wa Cuba aliyeongoza mapinduzi ya Kikomunisti, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, kakake ametangaza. "Amiri jeshi mkuu wa mapinduzi ya Cuba alifariki dunia mwendo wa saa 22… Read More
  • Watoto waliokamatwa wakifunzwa ugaidi waliweka njia panda jeshi la polisi Watoto wanne na wanawake wanne ambao jeshi la polisi liliwatia nguvuni kwa tuhuma za kujihusisha na mafunzo ya kigaidi maeneo ya Vikindu, Mkuranga mkoani Pwani, bado wanashikiliwa, huku upelelezi wa kina ukiendelea chini … Read More
  • Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na watumishi wa wilaya ya Kinondoni. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake katika wilaya Kinondoni ambapo asubuhi ya leo amezun… Read More
  • Trump amzungumzia Fidel Castro Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amesema kiongozi wa zamani wa Cuba Fidel Castro alikuwa "dikteta katili" saa chache baada ya Bw Castro kufariki dunia akiwa na miaka 90. Bw Trump amesema: "Leo, ulimwengu umeshuhudi… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE