January 12, 2016

Waziri wa Ajira, Kazi, Sera na Bunge, Jenista Mhagama amefuta leseni ya wakala wa ajira wa Kampuni ya SBC Tanzania, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji vya Pepsi jijini Mwanza baada kukiuka Sheria ya ajira na uhusiano kazini.

Pia, ameiamuru kampuni hiyo kumlipa kila mfanyakazi Sh50,000 kama faini ya kutokuwa na vifaa vya usalama kazini na kutotekeleza taratibu na sheria zilizowekwa na Idara ya Usalama na Afya Kazini (OSHA).

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Mwanza, pia alitoa siku 14 kwa kampuni hiyo kukamilisha vifaa vyote vinavyohitajika kwa wafanyakazi pamoja na kuwalipa stahiki zao.

Mhagama alitoa maagizo hayo jana alipofanya ziara katika kiwanda cha Pepsi na kukuta wafanyakazi 50 hawana vifaa hivyo.

“Nafuta kibali cha wakala wa ajira hapa kama utahitaji kuendelea na kazi hiyo uje wizarani ili kuomba upya,” alisema Mhagama.

Wakizungumza na gazeti hili leo, baadhi ya wafanyakazi hao walisema wanasafisha kreti moja ya soda yenye chupa 24 kwa Sh100 na kwamba, ikitokea wakavunja chupa hutakiwa kulipa.

Katika hatua nyingine, Mhagama alimtaka Mkurungezi wa Kiwanda cha Samaki cha Vickfish cha mjini hapa, kumlipa stahiki Yunis Marko kwa kufanya kazi bila kulipwa haki zake kwa mwaka mzima.

Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema ajira 35,000 zilizalishwa mwaka jana mkoani humo.

Ofisa Kiongozi wa Kituo cha Usuluhishi na Upatanishi wa Migogoro ya Kazi (CMA) mkoani Mwanza, Ephraim Lusega alisema kesi 566 za kazi ziliripotiwa kuanzia Januari mwaka jana hadi Desemba na 96 zilisuluhishwa au kuamriwa

Related Posts:

  • WATANZANIA WENGI WAFUNGWA HONG KONG Kasisi mmoja raia wa Australia amefichua na kuthibitisha kuwa kuna idadi kubwa ya wafungwa wenye asili ya Afrika katika magereza ya Hong Kong, wengi wao wakiwa ni kutoka Tanzania. Kasisi huyo John Wortherspoon ambaye … Read More
  • MWANA BLOG HOI KWA KIPIGO Mwanablogu Raif Badawi ana majeraha ambayo hayawezi kumruhusu kupewa adhabu nyingine  Saudi Arabia imeahirisha adhabu ya kumchapa viboko mwanablogu Raif Badawi kwa sababu ya afya yake. Mwanablogu huyo ambaye pia ni… Read More
  • MARKEL: TUTAWALINDA WAYAHUDI NA WAISLA,U UJERUMANI Kansela Angela Merkel   Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ameahidi kuwalinda Wayahudi na Waislamu wanaoishi nchini Ujerumani dhidi ya ubaguzi. Amesema demokrasia ndiyo njia bora ya kupambana na machafuko yanayo… Read More
  • PAPA AWASILI UFILIPINO Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani,Mtakatifu Francis, amewasili nchini Ufilipino, nchi yenye Wakatoliki wengi zaidi barani Asia, huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa. Maelfu ya Wafilipino wamejipanga katika misur… Read More
  • HUU NDIYO MPANGO MPYA WA THT 2015            Imezoeleka Tanzania House of Tallent (THT) imekua ikitoa wasanii peke yake ambao asilimia kubwa ya wasanii wengi wa Bongo Fleva wamepitia kwenye mikono ya Nyum… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE