Siku mbili zilizopita, kulisambaa na taarifa na kipande cha Video kikionesha kwamba, Bank ya NMB Tawi la Mbalizi jijini Mbeya , limevamiwa na majambazi na kuiba kiasi cha pesa na kisha majambazi hao kukamatwa na jeshi la polisi.
Kumbe tukio hilo halikuwa la kweli bali ni nini?
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya – Ahmed Msangi ametoa ufafanuzi kuhusu kipande cha video hicho kinachosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha uhalifu ukifanyika katika benki ya NMB tawi la Mbalizi Mkoani Mbeya na kueleza kuwa si tukio la ujambazi bali ni zoezi la polisi la kuonyesha jinsi ya kukabiliana na matukio ya ujambazi katika taasisi za fedha – mabenki nchini. Angalia video ya RPC Mbeya akitoa ufafanuzi
Hapa kamnda wa polisi mkoani Mbeya Hemed Msangi anafafanua
Kipande cha Video kikionesha tukio hilo
0 MAONI YAKO:
Post a Comment