January 28, 2016


 
Shirika la Afya Duniani WHO linaitisha kikao cha dharura kuamua iwapo kirusi cha Zika kitangazwe kimataifa kuwa ni kirusi hatari kwa afya. Katika mkutano maalum uliofanyika leo mjini Geneva, Mkurugenzi wa WHO, Margaret Chan, amesema kirusi hicho ambacho kimehusishwa na taathira za uzazi na matatizo ya ubongo kimekuwa kikienea katika hali ya kutisha. Kirusi hicho mara ya kwanza kiligundulikana hapo mwaka 1947 na kwa miongo mingi kimekuwa kikisababisha ugonjwa mdogo tu. Hata hivyo Dr. Chana amesema hali sasa imebadilika kabisa. Kwa mujibu wa kituo cha Marekani cha Udhibiti wa Maradhi, kirusi cha Zika hivi kiko katika nchi zaidi ya 20 hususan Amerika ya Kati na Amerika ya Kusini

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE