January 16, 2016

 

Diwani wa Ubungo Boniface Jacob kutoka CHADEMA ameibuka kidedea na ushindi wa kura 38 baada ya kushinda umeya na kumshinda mpinzania wake Benjamini Sitta wa chama cha Mapinduzi CCM aliyepata kura 20 Kinondoni jijini Dar es Salaam.Diwani wa Tandale (CUF) Jumanne Amir Mbunju amechaguliwa kuwa Naibu Meya. 
 DSC_0562 
Meya mpya wa Manispaa ya KinondoniBoniface Jacob akiwa mbele ya bara hilo jipya la Manispaa hiyo mapema leo mara baada ya kushinda kwa nafasi ya Umeya wa Kinondoni kwa kupata kura 38. Kulia kwake ni Naibu Meya, Jumanne Mbunju (CUF) ambaye pia ni diwani wa Tandale. Kushoto kwa Meya ni Mkurugezi wa Manispaa hiyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni  Bw.Charles Kuyeko

Kwa upande wa Umeya kwa Manispaa ya Ilala imechukuliwa na Charlse Kayoko  aliyeweza kunyakua kura 31 huku upande wa CCM Mgombea wake na wajumbe wake wakikimbilia ukumbi na kuambulia kura sifuri (0) na kwa upande wa Naibu Meya ikichukuliwa na Muba Omary (CUF) aliyepata (31) huku naibu aliyegombea naye kutoka CCM akipata kura sifuri (0).
Kwa hali hiyo Ilala na Kinondoni kwa sasa Mameya wake wanatokea  UKAWA huku uchaguzi mwingine unasubiriwa kwa hamu kubwa ni ule wa Meya wa jiji la Dar es Salaam unaotarajiwa kufanyika baada ya wiki moja.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE