January 16, 2016

Mwanamuziki wa muziki wa Rap kutoka Marekani kwa jina maarufu Mos Def ameamrishwa kuondoka Afrika Kusini katika kipindi cha siku 14 baada ya kukamatwa kwa kukiuka sheria za uhamiaji.

Mos Def anayejulikana kama Yasiin Bey alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Cape Town siku ya Alhamisi baada ya kujaribu kuondoka nchini humo na stakhabadhi bandia.

Idara ya maswala ya ndani imesema kuwa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 42 alitoa kile alichokitaja kuwa pasipoti ya dunia.

Imesema kuwa mwanamuziki huyo alikaa sana nchini humo kinyume na visa yake ya utalii aliyopata mwaka 2013.

Akiwa amezaliwa na kuitwa jina Dante Smith mjini New york,bwana Bey kwa sasa amepigwa marufuku nchini Afrika Kusini kwa kipindi cha miaka mitano,lakini amepewa haki ya kukata rufaa.

Cape Town

Amekuwa akiishi mjini Cape Town tangu mwezi May mwaka 2013 kulingana na vyombo vya habari nchini Afrika Kusini.

Akiwa ameteuliwa kuwania tuzo sita za Grammy,ameshiriki katika filamu kadhaa,ikiwemo The HitchHikers Guide to Galaxy,Be Kind Rewind na Italian Job.

Related Posts:

  • Aliyebaka mtawa akamatwa   Polisi nchini India wamemtia mbaroni mwanamume mmoja kuhusiana na ubakaji wa mtawa mmoja wa Kanisa Katoliki katika makaazi ya watawa Magharibi mwa Bengal. Viongozi wa Kikristo nchini India wamekosoa Serikali kwa k… Read More
  • Nay wa Mitego achukua maamuzi magumu kuhusu mtoto Nay wa Mitego na Mtoto wakeNay wa Mitego Amesikitishwa na Kauli ya Mzazi mwenzake SIWEMA ambaye wamezaa naye mtoto kwa kusema kuwa mtoto huyo si wa kwake bali ni wa aliyekuwa  Mpenzi wake wa zamani Obasanjo...Japo Wahen… Read More
  • CUF waitaka tume ya Taifa kukili kushindikana kwa kura ya maoni Naibu mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho ABDUAL KAMBAYA akizngumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam kuhusu mchakato mzima wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa kielecron… Read More
  • Magazeti ya leo hii March 26 haya hapa Leo Alhamisi Tarehe 26 March 2015. Tunakupatia fursa ya kutembelea kurasa za magazeti ya leo hii kama tulivyoyapata … Read More
  • Msilipize kisasa: Malim Seif Katibu Mkuu wa CUF taifa Maalim Seif amewaasa wanachama wa cuf jimbo la Dimani kutolipiza kisasi kwa kitendo cha kuchomewa moto ofisi yao usiku wa kuamkia juzi. Maalim Seif ambaye ni makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE