January 31, 2016

 

Licha ya kuwasili kwa mitambo  kusaidia zoezi la uokoaji wa kivuko kilichozama, zoezi hilo limeshindwa kufanyika kwa ufanisi kutokana na mvua kubwa iliyoanza kunyesha toka saa saba usiku hadi majira ya saa kumi jioni kukwamisha zoezi hilo pamoja na juhudi za kuvuta kivuko hicho kushindikana.

Hata hivyo huduma ya mawasilinao baina ya upande wa Ulanga na Kilombero imeweza kurejea mara baada ya Wizara ya mawasilinao ujenzi na uchukuzi kufanikiwa kutoa boti ambazo zimeanza kuvusha watu ili waendelee na safari.

Zoezi la uokoaji na uvutaji wa kivuko  ch MV Kilombero limezidi kuwa gumu, kutokana na changamoto ya vifaa vya uokozi, pamoja na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo  hilo, hivyo kukwamisha juhudi zinazoendelea kutolewa na mamlaka za uokozi.

Licha ya kutumia helkopta ya jeshi la Polisi kutafuta kama kuna watu ambao walisombwa na maji, juhudi hizo zimegonga mwamba.

 Hata hivyo juhudi zilizofanywa na wizara ya uchukuzi kwa kushirikiana na vikosi vya uokoaji kutoka kikosi cha wanamaji, vimefanikiwa kurudisha mawasiliano ya pande hizo mbili, kwa kuanza kuvusha wananchi wa kilombero na ulanga kwa kutumia boti za mwendo kasi. .

Wananchi wameiomba serikali kuongeza jitihada katika zoezi la uokoaji, na kuishukuru kwa kutoa boti ambazo zimeanza kuvusha watu.

Zoezi la kukitoa kivuko na kukivuta nchi kavu  limeshindikana kwa siku ya jana kutokana  na kunyesha kwa mvua hiyo pamoja na mitambo iliyopelekwa kuvuta, kushindwa kufanikiwa.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE