Serikali imesitisha zoezi la bomoabomoa katika maeneo mbalimbali isipokuwa katika eneo la bonde la mto msimbazi ambalo linaanzia katika vilima vya pugu hadi daraja la salender jijini Dar es Salaam ambalo hata hivyo litaendelea kwa utaratibu ambao hautaleta mateso na usumbufu kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo, waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira na muungano January Makamba amesema kwa sasa watakaohitajika kuhama ni wale tu ambao makazi yao yamo ndani kabisa ya bonde, kwenye miteremko ya kuingia kwenye bonde hilo pamoja na kwenye kingo za mto isipokuwa wale watakaokuwa na nyaraka halali walizopewa na mamlaka za umma ambao hawatahamishwa bila kupewa maeneo mengine ya kujenga ambapo watumishi wa umma waliowamilikisha watawajibishwa.
Hadi sasa nyumba 774 zimebomolewa kati ya hizo 20 zilifanyiwa uhakiki kuhusu uhalali wake na kubainika kuwa na hati na wakazi 119 walikuwa na leseni za makazi za muda mfupi ambao hata hivyo hawakuhamishwa.
Maamuzi hayo yamekuja baada ya kukutana mawaziri wanne wakiwemo wa waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi, waziri wa nchi, ofisi ya rais TAMISEMI, waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais pamoja na waziri wa Maliasili na Utalii ili tathmini zoezi hilo ambapo ripoti ya timu ya wataalamu kutoka wizara mbalimbali ilionyesha kuwa bonde la mto msimbazi imekamilika.
Aidha mkutano huo ulipokea taarifa kuhusu nyumba ya Mchungaji Getrude Rwakare juu ya zuio la kubomolewa ambapo baraza la mazingira limemfukuza kazi na kumfungulia mashtaka mwanasheria wake ambae amedaiwa kuwa ndio chanzo kushindikana kwa zoezi la kubomoa nyumba hiyo ambayo imejengwa mahali ambapo imezuia pasipostahili.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment