Zaidi ya shilling milioni 300 kushindaniwa
B
enki ya NMB imezindua mchezo wa bahati nasibu kwa wateja wake ambapo
watakuwa na nafasi ya kujishindia kuanzia shilingi 100,000/- hadi
shilingi milioni tatu 3,000,000/-. Bahati nasibu hiyo imepewa jina la
“Pata Patia” ambapo jumla ya shilingi milioni 300 zitashindaniwa.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa
Kitego cha Wateja Binafsi Boma Raballa alisema kwamba Promosheni ya Weka
Ushinde na NMB’ itakuwa na washindi kila wiki na kila mwezi na ni ya
kipekee ya wateja wa zamani na wapya
Bw. Raballa aliongeza kuwa ” Wateja watatakiwa kuweka fedha katika
akaunti yoyote ya NMB kiasi cha chini kikiwa ni Shilingi elfu hamsini
(50, 000) ili kupata nafasi ya kushinda na zaidi uwekavyo fedha utapata
nafasi zaidi ya kushinda. Wateja wanaweza kuweka fedha kupitia tawi letu
lolote, NMB Wakala na NMB mobile.”
Promosheni hii itakuwa na droo za kila mwezi ambapo tawi husika la
benki ya NMB litawasiliana na washindi 24 kila mwezi kuzungusha gurudumu
la bahati katika matawi yaliyochaguliwa na NMB.
NMB imetenga jumla ya shilingi milioni 300 kushindaniwa. Washindi 144
ambao ni wateja wa zamani na wapya wanaweza kushinda hadi shilingi
3,000,000/= kila mmoja; jumla ya washindi 24 watabainishwa kila mwezi
kwa kipindi cha miezi sita.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment