Mwanamuziki mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili akicharaza nyuzi za Gitaa lake chini ya Kundi zima la Mjomba Band.
MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili
amefariki dunia akiwa chumbani kwake, Tabata jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi (CHAMUDATA) Hassan Msumari,
amesema kuwa kifo cha Mapili kimegunduliwa usiku huu baada ya mlango wa
chumba chake kuvunjwa.Mlango huo ulivunjwa baada ya Kassim Mapili kutoonekana tangu alipokwenda kutazama mpira wa Arsenal na Barcelona Jumanne usiku.Kwa mujibu wa Msumari, mara mlango ulipovunjwa Kassim Mapili
alionekana akiwa ameshafariki akiwa amejifunga taulo, ishara
inayoonyesha kuwa aidha alikuwa anakwenda kukoga au ametoka kukoga.Jumatatu jioni Kassim Mapili alishiriki vizuri mazishi ya mwanahabari
Fred Mosha makaburi ya Kinondoni ambapo alipewa wasaa wa kuongea
machache na kama vile hiyo haitoshi, Mapili aliimba makaburini hapo
kuomboleza kifo cha Fred Mosha.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment