Producer maarufu kutoka Marekani Scott Storch, aliyetengeneza hits za mastaa kadhaa wakiwamo Rick Ross na Chris Brown, amemshambulia mtayarishaji wa muziki kutoka studio za Fishcrab Tanzania, Lamar kisa kapost kipande cha beat yake.
Ilikuwa majira ya usiku wa jana Lamar alipost clip ya beat hiyo ya Scott na kumtag kama miongoni mwa watu wanaomuhamasisha kikazi.
Scott alionesha ghadhabu na kucoment kwenye post hiyo akimuuliza Lamar kwanini anapost beat yake?. Lamar alimueleza vizuri tu kuwa anahamasika na kazi za Scott na anamuangalia kama watu anaofata nyendo zao.
Mmarekani huyo akamtaka Lamar aache kufanya hivyo ambapo alijibiwa ‘sawa kaka’.
Watanzania kadhaa wakiwamo wasanii Julio Batalia, Dogo Janja na Lucci wamemshukia Scott kwa kutothamini heshima anayopewa na maproducer wanaochipukia.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment