February 04, 2016

                              
Serikali  imesema tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini linatokana na uchakavu na kuzidiwa kwa vituo vya kupoza umeme na miundombinu ya usafirishaji na usambazaji nishati hiyo.

Katika kukabiliana na tatizo hilo Tanesco inachukua hatua za kujenga mifumo ya njia kubwa za umeme wa msongo wa kilovoti 400 (Iringa- Dodoma-Singida-Shinyanga), gridi ya Kaskazini Mashariki (Dar es Salaam, Chalinze,Tanga –Arusha), ya Kaskazini Magharibi (Geita- Kagera –Katavi- Kigoma- Rukwa na Mbeya) na Makambako- Songea wa kilovoti 220.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani wakati akijibu swali la Mbunge wa Magu, Boniventure Kiswaga (CCM). 

Kiswaga alitaka kufahamu serikali imejipangaje kukabiliana na tatizo la kukatika katika kwa umeme.

Pia mbunge huyo alitaka kufahamu, Je serikali itakamilisha lini kupeleka umeme katika vijiji vya jimbo hilo ikizingatiwa mpaka sasa ni asilimia 20 tu ya vijiji ndiyo vina umeme. 

Kalemani akijibu swali hilo, alisema tatizo la kukatika kwa umeme linatokana na uchakavu na kuzidiwa kwa miundombinu ya kupoza umeme pamoja na matukio ya kulipuka kwa transfoma yanayosababishwa na radi hasa kipindi cha mvua pamoja na wizi wa mafuta ya transfoma unaofanywa na wananchi wasio waaminifu.

Alisema Tanesco inakamilisha upanuzi wa usambazaji wa umeme katika majiji makubwa ya Arusha, Dar es Salaam, na Mwanza ambapo kazi hizo zitahusisha ujenzi wa njia mpya za umeme na kupanua vituo vya kupoza umeme.

“Kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro kumeimarisha upatikanaji wa umeme maeneo ya Mirerani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA),” alisema Kalemani.

Pia vituo vya kupoza umeme katika jiji la Dar es Salaam vya Gongo la Mboto, Kipawa, Mbagala, na Kurasini vitaunganishwa kwa njia ya sakiti mzunguko kutoka Ubungo na Kinyerezi kuanzia Machi mwaka huu

Related Posts:

  • Maandalizi ya tamasha la miaka 10 ya THT, yakamilika Escape 1 Tamasha la miaka kumi ya THT litakalofanyika jumamosi hii katika viwanja vya Escape 1 Mikocheni, limekamilisha maandalizi yake na hivyo kuwataka wadau na wapenzi wake wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani kubwa ya m… Read More
  • 26 Wauawa Kigaidi nchini Misri   Takriban watu 26 wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wapiganaji la Islamic State Kaskazini mwa Misri katika eneo Sinai Gari lililokuwa na mabomu lilipiga kituo cha kijeshi kaskazini… Read More
  • Baba ajiua kutokana na picha za mwanawe    Baba mmoja amejiua baada ya kuona picha za uchi zamwanawe wa kike katika jarida la Playboy nchini Romania. Loredana Chivu alirarua ukurasa uliokuwa na picha yake akiwa 'amepos' katika jarida hilo la Playboy … Read More
  • Hukumu ya Cheka miaka mitatu jela, maoni ya wadau haya hapa    Siku ya jana Th 2 Febr 2015, tasnia ya burudani ilipata pigo baada ya bondia francis cheka kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na fidia ya Shilingi milioni moja kufuatia kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumpi… Read More
  • Ukweli Kuhusu Tevez Aliyekatwa Uume HABARI ZA UHAKIKA JUU YA SAKATA LA JUMAANNE TEVEZ. Nikweli kwamba huyu bwana yuko South Africa Pretoria. Bwana Tevez alodhaminiwa mzigo na vijana wenzake huko Bondeni kwamba akauze kisha alete Mpunga. Mdhamini alikuwa n… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE