February 04, 2016

                        
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananch UKAWA, Mh. Edwrad Lowassa amesema ni vema serikali ikahakikisha inapata suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio machi 20 mwaka huu.

Mh. Edward Lowassa amesema hayo ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na wazee kutoka chama cha Chadema ambapo amesema  anaunga mkono uongozi wa CUF kutokushiriki uchaguzi huo huku akisisitiza endapo serikali ikishindwa kumaliza mgogoro huo kabla ya mach 20 huenda hali ya kisiasa Zanzibar ikabadilika.

 

Aidha amewahakikishia wazee hao kuwa yeye na uongozi mzima wa UKAWA wako imara katika kuhakikisha wanatetea maslahi ya watanaznia ambapo pia amemshukuru waziri mkuu kwa kuruhusu mikutano suala ambalo linawapa fursa ya kuajipanga ili kuwashukuru watanzania waliojitokeza kupiga kura mapema 25 ,huku pia akiigusia katiba ya Tanzania.

 

Kwa mujibu wa risala ya wazee hao iliyosomwa na mzee Enec Ngombare wamempongeza Mh. Lowassa kwa na uvumilivu wake baada ya uchaguzi ambapo pia wamemhakikishia kuwa wako pamoja nae katika safari ya kuelekea mwaka 2020.

 

Katika mkutano huo pia uliohudhuliwa na kada wa siku nyingi Kingune Ngombare Mwiru, Mh Lowassa amewataka wazanzibar na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu na kuhakikisha wanadumisha amani ya nchi hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wanaendelea na juhudi za kutafuta suluhu ya kisiasa visiwani Zanzibar.

 Source: ITV

Related Posts:

  • Mtoto wa Pele afungwa jela miaka 33 Brazil 23 seconds ago Gwiji wa soka Pele akionekana mwenye huzuni. Akiwa na umri wa miaka 43, mchezaji mpira mstaafu, atatumikia kifungo kwa kosa la kujipatia p… Read More
  • MAMI YA WATU MOROGOR WAUAGA MWILI WA MTOTO NASRA RASHIDI         Safari ya Mwisho ya Nasra.kutoka hospitali ya mkoa wa Morogoro hadi Jamhuri stadium na baadaye Makaburi ya Kolla.Tunaamini sisi tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi.alikuon… Read More
  • RAY C ALITAMANI PENZI LA KIKONGWE MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema kwa sasa hana mpango wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu, na kama ikitokea basi atamtaka kuwa na miaka kuanzia 60. Akizungumza kat… Read More
  • MAJAMBAZI YAUA ARUSHA Mwananchi mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi eneo na Clock Tower jijini Arusha. Majambazi hao walikuwa wakipora kwenye Bureau De Change iitwayo Nothern ambapo mareh… Read More
  • MAMA YAKE ZITTO KUZIKWA KIGOMA KESHO    Mzee Stephen Wassira akimpa Zitto pole na faraja katika msikiti wa Maamur.Picha kwa hisani ya Khalfan Said. Maiti ya Bi Shida Salum, mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, imesaf… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE