March 21, 2016

 

 

Mwanadada Mkali kwenye Bongo fleva DAYNA NYANGE leo ameweka wazi aliyokuwa nayo moyoni kumuhusu mkali mwenzake wa muziki hapa Bongo ALI KIBA



Dayna anasema hajakuwa kwenye uhusiano mzuri na Ali kiba na haelewi sababu, kwani amekuwa akimpotezea pindi akiomba kufanya nae kazi,


"Daaah Ali Kiba kiukweli ni msanii ninaye mkubali sana hapa bongo tangu kitambo, ila tatizo linakuja kati yetu ni nakumbuka kipindi cha nyuma nilipokuwa nafanya nyimbo ya NIVUTE KWAKO nilimuomba tufanye wote, nilimtafuta sana bila mafanikio kila nikimpigia alitaka niongee na uongozi wake, nilipompata sikuridhishwa na alichokifanya ndio maana nikamuweka Barnaba." Alisema Dyna



Mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na singo yake ya #ANGEJUA alimaliza kwa anahisi Ali Kiba na yeye damu zao haziendani,


"Mara ya pili tena nakumbuka nilimtafuta tufanye kazi, ilikuwa ni nyimbo yangu #LEO niliyoifanya na BLUE ilikuwa nifanye na Kiba pia ila nilipokuwa nampigia simu alinikwepa na kutaka niongee na menejimenti yake. Sasa sifahamu kwa nini alikuwa anafanya vile, nahisi damu zetu tu haziendani."-@daynanyange

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE