March 21, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amewataka wanachama wenzake wa Chama Cha Mapinduzi CCM,kuiacha Demokrasia ichukue mkondo wake katika suala la uchaguzi wa meya wa jiji la Dar es Salaam kwa kuwa asiye kubali kushindwa si mshindani.



" Suala la umeya Dar es salaam liachwe demokrasia ichukue mkondo wake. Na niwaombe wana CCM wenzangu tusilazimishe mambo, tukubali kushinda lakini pia tukubali kushindwa. Mahali tunapostahili kushinda kama tumeshinda basi tushinde kweli. Lakini mahali tunaposhindwa basi tukubali kushindwa na hiyo ndiyo Demokrasia ya kweli. Akishinda mwana CCM ni sawa, akishinda wa CHADEMA ni sawa....sisi tunachotaka ni maendeleo ya watu wa Dar es salaam"- Alisema Rais Magufuli


 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE