March 21, 2016


Mwandishi wa habari Salma Said aliyedaiwa kutekwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam amepatikana na kuangua kilio mbele ya waandishi wa habari akieleza namna alivyodhalilishwa na kupigwa na watekaji hao.

Taarifa za kutekwa kwa mwandishi huyo wa shirika la utangazaji la Ujerumani na gazeti la Mwananchi ilianza kujulikana mnamo tarehe 18  March 2016 mara tu baada ya kutekwa na watu wasiojulikana akiwa anatokea Zanzibar kuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu yake ili kesho yake aweze kurejea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa marudio,tukio ambalo ilizua mijadala katika mitandao ya kijamii na kusababisha watu kuzungumza mengi.


Hata hivyo mwandishi huyo ambaye amejikita katika habari za kutetea haki za binadamu na habari za siasa ameeleza alivyopigwa na watekaji hao bila huruma huku nia yao ikionekana ni kumzuia kushiriki uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar.
Video yake ipo hapa chini
 
                   

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE