MJUKUU wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Abeid
Amani Karume, amepinga hatua ya kumtangaza Dk. Alli Mohammed Shein, kuwa
rais Visiwani
Fatma Amani Abeid Karume, mtoto wa kwanza wa rais mstaafu, Amani Abeid Karume amesema, “Dk. Shein, siyo kiongozi halali wa Zanzibar. Amewekwa madarakani na jeshi na kinyume na Katiba na taratibu za nchi.”
Amesema, “Rais aliyewekwa madarakani na vyombo vya dola, siyo rais wa
wananchi. Rais anayewekwa madarakani kwa nguvu za kijeshi na vitisho,
hawezi kuwa rais wa wananchi. Anakuwa rais wa majeshi.”
Akiongea kwa sauti ya uchungu na MwanaHALISI Online, Jumatano wiki
hii, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Fatma amesema, “Chama Cha
Mapinduzi, kisijidanganye. Zanzibar siyo shwari. Kinachotengenezwa sasa,
siyo utawala. Ni muendelezo wa chuki, visasi na uhasama.”
Amesema, “CCM ya Tanganyika, ndiyo inayoiharibu Zanzibar.
Wanalazimisha viongozi wasiokubalika na wananchi Visiwani kutawala kwa
manufaa yao binafsi.”
Soma mahojiano kamili na mwanasheria huyo mashuhuri nchini, katika gazeti la MwanaHALISI Jumatatu wiki ijayo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment