Zubery alimfanyia dua hiyo Makonda Dar es Salaam jana asubuhi alipofika nyumbani kwake kujitambulisha na kumjulia hali pamoja na kumueleza mambo kadhaa ya maendeleo yaliyofanyika.
"Tunakuomba
mola wetu kuwapa moyo wa imani na uzalendo na kuwaepusha na mabaya
yote Mkuu wetu wa Mkoa Paul Makonda, Rais wetu Magufuli pamoja na
viongozi wote ili waliongoze taifa letu kwa amani" alisema Mufti Zubery" wakati akiomba dua hiyo.
Makonda
akizungumza na Mufti Zubery nyumbani kwake Mikocheni alimwambia kuwa
kuna mambo kadhaa ameyafanya kwa kushirikiana na watendaji wenzake kwa
kukutana na waendesha boda boda ili kuwawezesha kupata mkopo
utakaowasaidia kupata vitendelea kazi zao kama kupata kofia ngumu mbili
za kuvaa dereva na abiria wake ili kuwasaidia katika shughuli zao za
kusafirisha abiria.
Makonda
alitaja mambo mengine kuwa ni suala zima la kupambana na uhalifu ambao
bado unaonesha kupamba moto hasa ujambazi wa kutumia silaha za moto.
Alitaja
mambo mengine kuwa ni mkutano alioufanya hivi karibuni wa kukutana na
wenyeviti wa mitaa na maofisa watendaji ili kuzungumzia suala la
utunzaji wa mazingira na mambo mengine ambapo alisema ameandaa mpango wa
kumzawadia mwenyekiti atakayefanya vizuri kwenye mtaa wake.
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema jambo
alilofanya Makonda la kumtembea Mufti ni jambo zuri na kuwa kumuona
mufti ni sawa kama amewaona waislam wote nchini.
Alisema
wanamuombea Makonda mungu amzidishie wepesi katika kazi zake kwani ni
viongozi wachache wanaopata madaraka ambao uwakumbuka viongozi wa dini
kama alivyofanya Makonda.
Katika
hatua nyingine Makonda alifanya ukaguzi wa barabara kadhaa za Manispaa
ya Kinondoni ambazo hivi karibuni aliagiza zifanyiwe marekebisho ikiwa
ni pamoja na kuchimba mifereji baada ya kuharibika kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha.
Mufti Zubery, akifanya mazungumzo na Makonda.
Dua ikiendelea nyumbani kwa mufti Mikocheni.
Makonda akiagana na Sheikh Abubakar Khalid na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment