
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Makete
Mh.Noramn Sigalla wakati alipowasili kwenye shamba la Kitulo ambalo ni
moja ya Mashamba makubwa ya kufuga Ng'ombe wa kisasa aina ya Mitamba.


Huwa
ni mfano wa Ng'ombe wa kisasa aina ya Mitamba wanaopatikana shamba la
kitulo wenye uwezo wa kutoa maziwa lita 15 hadi 20 wanapokamuliwa mara
moja kwa
kila mmoja
.

Mwigulu
Nchemba akipewa maelekezo kutoka kwa meneja wa shamba la kitulo
kuhusiana na uzalishaji wa Ng'ombe aina ya mitamba.Kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya
Makete
.

Mh.Mwigulu
Nchemba akiwa kwenye shamba la kitulo akipewa maelezo mbalimbali
yanayohusiana na kuyumba kwa ufugaji wa ng'ombe kwenye shamba hilo.

Moja
ya Farasi ambaye anafugwa kwenye shamba la Kitulo,Idadi ya Farasi
wanaofugwa imepungua kutokana na wengi kuuzwa kwa wananchi.

Moja ya Dume la Ng'ombe la kisasa ambalo limezalishwa Shamba la kitulo.

Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia namna ukamuaji wa maziwa unavyofanyika kwenye shamba la kitulo
.

Akiwa
njiani kutokea shamba la Kitulo,Mh.Mwigulu Nchemba alipata nafasi ya
kuzungumza na wananchi wa kata ya kikondo ambao walikuwa na malalamiko
ya kulipwa fidia baada ya kuhamishwa kutoka hifadhi ya Kitulo,Madai yao
ya fidia ni fedha ya Tanzania Bilion 1.8,Mwigulu amewaahidi kuwasaidia
wananchi hao kwa kuzungumza na waziri wa Mali asili na Utalii aweze
kuprocess malipo hayo.

Mbunge
wa Makete,Dr.Norman Sigalla akiomba kwa Waziri wa kilimo,Mifugo na
Uvuvi kufanikisha zoezi la kuboresha shamba la kitulo ili uchumi wa
wananchi wake wa Makete na wanaozunguka shamba hilo uimarike.
Shamba la Kitulo la Ufugaji wa Ng'ombe
aina ya Mitamba lilianzishwa mwaka 1963 na Mwl.Nyerere kama eneo la
kuzalisha maziwa ya kusambaza nchi nzima,Ng'ombe aina ya Mitamba
wanaopatikana kwenye shamba hilo waliingizwa nchini kutokea Marekani na
nchi za Ulaya Mashariki ambazo hali yake ya hewa inaendana na ile ya
kitulo ambayo kuna wakati ni 0 centgrade,na hali ya juu zaidi inaweza
kuwa 19 Centgrade.
Kuanzia miaka hiyo ,Shamba la kitulo
ambalo linauwezo wa kulisha ng'ombe elfu nne (4000),Shamba hilo kwa sasa
lina ng"ombe mia saba tu(700).
Mbali zaidi,nyenzo za kutunzia ndama na
kukamua maziwa haziridhishi na ukuziaji wa nyasi zilizopandwa kwaajili
ya malisho haulidhishi.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi
Mh.Mwigulu Nchemba,baada ya kusikiliza na kuona changamoto
zinazolikabili shamba la kitulo kwa ufugaji wa ng'ombe,Ameahidi
kuhakikisha analiboresha na kusaidia upatikanaji wa ng'ombe wa
kutosha,huduma za kutosha ili eneo la kitulo liwe ni shamba darasa hata
kwa mashamba mengine ndani na nje ya nchi yetu.
Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment