March 05, 2016

Kiongozi wa upinzani nchini Sudan afariki dunia
Dakta Hassan al-Turabi, kiongozi na shakhsia muhimu wa upinzani nchini Sudan amefariki dunia.
Hassan al-Turabi aliaga dunia jana katika hospitali moja mjini Khartoum akiwa na umri wa miaka 84. Ripoti zinaeleza kuwa, mwanasiasa huyo mkongwe nchini Sudan alifariki dunia kutokana na shinikizo la moyo. Bwana Turabi alikuwa mshirika wa karibu wa Rais Omar Hassan al-Bashir wakati alipochukua madaraka kupitia mapinduzi lakini wakakosana muongo mmoja baadaye.
Licha ya umri mkubwa na uzee, katika miaka ya hivi karibuni, kiongozi huyo wa upinzani alikuwa akitiwa mbaroni mara kwa mara na kushikiliwa kifungoni.
Licha ya mashinikizo na kuandamwa mara kwa mara na serikali ya Rais al-Bashir, lakini mwanasiasa huyo hakuacha kumkosoa Rais al-Bashir.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE