Leo March 4 2016 Kampuni ya Jamii Media inayoendesha JamiiForums.com na Fikrapevu.com
imejitosa kutetea kile inachokiita ni kunyimwa haki ya wananchi kupata
taarifa na kulindwa kwa uhuru wao wa maoni na kujieleza unaolindwa kwa
mujibu wa katiba ya Nchi.
Jamii Media wameamua kufungua shauri Mahakama kuu kutaka kifungu cha 32 na 38 cha sheria ya Makosa ya Mtandao viangaliwe upya, akizungumza kwa niaba ya Jamii Media wakili Shukuru Mlwafu ameeleza…
>>>‘baadhi
ya vifungu vya sheria ya kimtandao vinakiuka masharti ambayo yamewekwa
na katiba hasahasa vinaingilia haki ya faragha ambayo wateja wetu wanayo
kikatiba, njia pekee ni kufungua shauri la kikatiba kupinga vifungu
hivyo na kuiomba mahakama ibatilishe na itamke kuwa vifungu hivyo ni
batili kwa kuwa vinaenda kinyume na ibara 16 na 18 ya katiba’ ;- Shukuru Mlwafu
Hatua hiyo
ya kufungua shauri Mahakamani imekuja baada ya kuwepo na shinikizo
kutoka Jeshi la polisi kuwataka Jamii Forum kutoa taarifa za baadhi ya
wateja wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Maxence Melo amesema..
>>>’kuanzia
uchaguzi october 2015 kumekuwa na barua kadha wa kadha zinazotaka
kupata taarifa za siri za wanachama wa mtandao wa jamii forum kitu
ambacho tunahisi hata mitandao mingine ya kijamii wanafanyiwa na
kumekuwa na mashinikizo kadha wakadha wakitaka tutoe IP Address za
wateja, majina halisi na hata maeneo waliopo sasa tunaona hii itapekea
kuvunjwa kwa haki ya watumiaji wa Jamii forum’:-Maxence Melo
Source:Millardayo.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment