
Kituo cha Madungu Chake-Chake, Pemba wapiga kura hawajafika. Ni maafisa tu wa tume na maafisa wa usalama walio kituon. picha na BBC
Maafisa wa usalama wakishika doria mjini Chake kisiwani Pemba.
Kumbuka, Chama cha Wananchi (CUF) kilitangaza kwamba hakitashiriki uchaguzi wa marudio unaoendelea leo. Chama hicho kinaamini kilishinda uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na mgombea wake Maalim Seif Hamad anafaa kutangazwa mshindi.
Tume ya uchaguzi Zanzibar hata hivyo ilitangazwa kwamba hakuna aliyejiondoa rasmi kutoka kwa uchaguzi wa leo.

Kituo cha Madungu Shule ya Msingi...Pemba. Picha kutoka kwa Askofu Tza

Rais wa Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein amepiga kura katika Kituo cha shule ya Msingi Kibele mapema leo asubuhi. picha kwa hisani ya Cloudsfm Tz
Safari zote za meli kati ya bandari ya Dar es Salaam na visiwa vya Zanzibar zimekatizwa.
Wapiga kura kituo cha Bungi, Unguja wasubiri kituo kifunguliwe.
Tutaendelea kuwajuza kadiri tutakavyopata habari
0 MAONI YAKO:
Post a Comment