Takriban watu 14 wameuawa wakati basi
moja lililokuwa likisafirisha wanafunzi wa kigeni kuhusika kwenye ajali
ya barabarani katika barabara kuu nchini Uhuspania kati ya miji ya
Barcelona na Valencia.
Wengi kati ya watu 57 waliokuwa ndani ya
basi hilo walikuwa ni wanafunzi waliohudhuria mpango unaojulikana kama
Erasmus, na walikuwa wakirejea kutoka Barcelona baada ya kuhudhuria
warsha ya kufyatua fataki.
Ajali hiyo ilitokea karibu na eneo la Freginals kilomita 150 kusini
mwa Barcelona. Uraia wa wale waliuawa na 43 waliojeruhiwa
haujathibitishwa wala kile kilichosabisha ajali hiyo.
Waziri wa
masuala ya ndani wa eneo la Catalonia Jordi Jane alisema kuwa dereva wa
basi aligonga kifaa upande wa kulia ambapo basi likaelekea upande wa
kushoto na kisha kugonga gari llilokuwa likitokea upande mwingine.
Dereva wa basi hilo alinusurika ajali hiyo na amepelekwa katika kituo cha polisi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment