
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), David Mattaka, amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuliingizia serikali hasara ya Dola za Marekani 772,402.08.
Akisoma
mashtaka hayo jana, Vitalis Thimos, wakili wa serikali mbele ya
Respicius Mwijage, Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu alisema kuwa,
mshtakiwa huyo anakabiliwa na kosa hilo kutokana na matumizi mabaya ya
madaraka katika ofisi ya umma.
Tuhuma
hizo ni pamoja na kutia saini mkataba wa kukodisha ndege aina ya Air
bus A320-214 kwa Kampuni ya Wallis TradingInc bila kufuata sheria na
taratibu za zabuni.
Mattaka
anadaiwa kuiingizia hasara serikali kutokana na hatua yake ya
kuidhinisha pesa za matengenezo ya ndege hiyo katika Kampuni ya
AEROMANTENIMIENTO.
Hasara nyengine ni matumizi mabaya kwa kununua vifaa vya ndani ya ndege hiyo yaliyoigharimu Dola za Marekani 35,984.82.
Watuhumiwa
wengine kwenye kesi hiyo ni Ramadhani Mlinga, Mkurugenzi wa Manunuzi
ATCL na Bertha Soka ambaye ni mwanasheria wa shirika. Watendaji hao
wanadaiwa kushindwa kuzuia ubadhilfu huo. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe
19 Machi.
Source:http:mpekuzihuru.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment