March 16, 2016

                      
Meli ya China iliozamishwa na walinzi wa pwani ya Argentina

Walinzi wa pwani nchini Argentina wamesema kuwa wameifukuza na kuizamisha boti moja ya Uchina iliokuwa ikivua samaki kinyume cha sheria katika maji ya taifa hilo siku ya Jumatatu.

Katika taarifa ,walinzi hao wa pwani wamesema kuwa mojawapo ya boti hizo iliionya boti hiyo ya Lu Yan Yuan Yu 010 kwa kuifyatulia risasi iliopukwa ikielekea katika maji ya kimataifa.

Walinzi hao wanasema kwamba waliionya kupitia kipaza sauti.

Wafanyikazi wote 32 wa boti hiyo waliokolewa.

Uchina imeonyesha wasiwasi wake kuhusu kuzamishwa kwa boti hiyo.

Msemaji wa wizara ya kigeni wa taifa hilo Lu Kang alisema katika taarifa kwamba Beijing imewasilisha wawakilishi wake nchini Argentina ikitaka uchunguzi kamili kufanywa kuhusiana na kisa hicho.

Uvuvi haramu ni tatizo la kawaida katika eneo hilo.

Mara nyingi boti zinazopatikana zikifanya uovu huo hutafuta mbinu za kugongana na walinzi hao na hivyobasi kuhatarisha sio maisha ya wafanyikazi wake bali hata yale ya walinzi hao wa pwani,ambao waliamrishwa kuifyatulia risasi meli hiyo,taarifa hiyo ya walinzi wa pwani hiyo walizungumza kwa lugha ya kihispania.

Hatua hiyo inajiri licha ya uhusiano wa Argentina na Uchina kuimarika katika siku za hivi karibuni.

Related Posts:

  • Brand New Video: Medybotion ft Mash Jay New video release for MEDYBOTION Song Tittled KANIVUMIALIA Song Was Produced By VENNTSKILLZ For KWANZA RECORDS Video Was DIRECTED BY GQ Video Was Shot In MOROGORO TANZANIA EAST AFRICA MEDYBOTION INST… Read More
  • Siogopi kufungwa – Rais Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema atawatetea Watanzania kwa nguvu zake zote juu ya majizi huku akisema haogopi kufungwa badala yake majizi ndio yatakayo fungwa. Rais Mgufuli ames… Read More
  • Mwana FA na AY, Kulipwa bilioni Mbili za Tigo Hatimaye ile kesi ya wanamuziki AY na Mwana FA, walioishtaki kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa kutumia nyimbo zao bila makubaliano nao, imefika tamati. Katika hukumu iliyoamliwa na mahakam kuu, Kampuni ya Tigo inatak… Read More
  • Mtoto wa Future na Ciara apata dili   Mtoto wa rapper Future na mwanamuziki Ciara, Zahir Wilbur ambaye kwa sasa analelewa na mama yake pamoja na baba yake wa kambo Russel Wilson, amepata dili lake la kwanza la kuingiza fedha nyingi. Zahir ambaye a… Read More
  • Siwezi kujiunga ROCKSTAR4000 kwa MKUBW FELLA pananitosha - Chege Chigunda   Mwanamuziki toka katika kundi la Wanaume Chege Chigunda mtoto wa Mama Saidi, amesema yeye awezi kujiunga na ROCKSTAR4000 kwani kwa mkubwa Fella panamtosha sana. Chege Chigunda amezungumza hayo alipofanya Interview … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE