Klabu ya wekundu wa msimbazi SimbaMarch 16 kupitia kwa mkuu wao wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyoHaji Manara wametangaza maamuzi mapya kuhusu nahodha wao msaidiziHassan Is-haka waliyekuwa wamemfungia kwa muda usiojulikana.
Simba wametangaza kumpunguzia adhabu Hassan Is-haka na kwa sasa atapata adhabu ya kufungiwa mwezi mmoja, kupokea nusu mshahara na kuvuliwa unahodha msaidizi, maamuzi hayo yamekuja baada ya kocha wa SimbaJackson Mayanja kuomba apunguziwe adhabu mchezaji huyo.
Kutoka kushoto ni kocha wa SimbaJackson Mayanja, Haji Manara
Is-haka alifungiwa kwa muda usiojulikana na Simba baada ya kumtolea kauli mbaya kocha wake Jackson Mayanja. Hata hivyo Simba pia wametangaza kuwa wataishitaki TFF kwa waziri wa habari, michezo, sanaa na utamaduni Nape Nnauye kutokana TFFkuahirisha sana mechi za Yanga na Azam FC, hivyo ni sawa na kupanga matokeo.
Source:Millardayo.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment