March 15, 2016

Mtawa 
 Mother Teresa alikuwa mtawa wa kanisa Katoliki 


 Papa 
Mother Teresa na Papa John Paul II wakiwa Kolkata, India tarehe 3 Februari 1986


Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametangaza kwamba Mother Teresa atafanywa mtakatifu Septemba mwaka huu.
Sherehe ya kumtawaza kuwa mtakatifu itafanyika tarehe 4 Septemba.
Njia ya kumfanya mtakatifu ilifunguliwa Desemba mwaka jana baada ya Vatican kutambua muujiza wa pili uliohusishwa naye. Muujiza huo alipokea mwanamme raia wa Brazil ambaye alipona saratani kwenye ubongo wake.
Mother Teresa alipewa tuzo ya amani ya Nobel kutokana na huduma yake kwa raia maskini kwenye vitongoji vya jiji la Calcutta nchini India.
Alizaliwa 1910 eneo ambalo kwa sasa hujulikana kama Macedonia na wazazi wa asili ya Albania na kupewa jina Agnes Gonxha Bojaxhiu.
Alipewa uraia kamili wa India baada ya kuanzisha kikundi cha watawa cha Missionaries of Charity mwaka 1950.
Alifariki 1997 akiwa na umri wa miaka 87. Alifanywa mbarikiwa mwaka 2003.

Related Posts:

  • Official VIDEO: Star Boy Wizkid na Mut4y - Manya African star Boy kama anavyofahamika na wengi mwanamuziki Wizkid kutoka nchini Nigeria, ameachia video yake mpya ya wimbo unaitwa Manya akiwa na mwanamuzik Mut4Y . Anakupa muda wa kuitazama hii video hapa hapa . Bofya … Read More
  • Official Music Video: Aslay - Hauna   Aslay kwa sasa ndiyo mwanamuziki anayeongoza kwa kuachia nyimbo zake mfululizo. Kila kukicha Aslay anathibitisha kipaji chake kilivyo cha hali ya juu. Eti wengine wanasema aliondoka na daftari la nyimbo wakati kund… Read More
  • Wazanzibar waiomba Fiesta ifike visiwani Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahamud ametumia kongamano la Fursa iliyoandaliawa na Clouds Media Group kuomba tamasha kubwa la muziki la Fiesta lifike kisiwani hapo. Hayo yamebainishwa leo na RC Ayoub … Read More
  • New Audio: Msaga sumu x Man Red Red Mfalme wa Singeli Tanzania Msaga Sumuj, ametuletea wimbo mpya unaitwa Vyuma vimekaza. Msaga hapa amemshirikisha mwanamuziki Man Red Red    … Read More
  • Hii Ndiyo penati iliyoipa Yanga goli la 3 Mpira umemalizika katika uwanja wa Taifa. Matokeo ni Yanga wameifunga Mbeya City Magoli  5 kwa Sufuri. Tazama Goli la tatu la Yanga lililofungwa kwa mkwaju wa Penati        &… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE