March 16, 2016

                         
Mkuu Mpya wa Mkoa wa dsm Paul makonda ametoa saa 24 kwa watendaji wote wanaosimamia idara mbali mbali katika Manispaa za halmashauri ya jiji la dsm kueleza Utekelezaji wao wa majukumu tangu walipopewa majukumu katika idara hizo.

Bw,Makonda ambaye ameteuliwa hivi karibuni akitokea katika Halmashauri ya manispaa ya kinondoni ambapo alikuwa Mkuu wa wilaya ametoa agizo hilo mara tu alipofika katika Ofisi mpya ya mkuu wa mkoa ilizopo Ilala boma ambapo alikutana na wakuu wa wilaya za temeke,ilala pamoja na katibu tawala wa mkoa wa dsm na wakuu wa idara kutoka halmashauri ya jiji la dsm.

Amesema ameteuliwa na Dr.John Magufuri ili ahahakikishe jiji la dsm linakuwa katika hadhi inayokubalika ,watendaji na wakuu wa idara waache kufanya kazi kwa mazoea huku akiwatahadharisha kuwa kasi ya utendaji wa awamu ya tano haiwezi kumvumilia mtendaji yeyote atakayeshindwa kusimamia majukumu aliyopangiwa ya kuwatumikia wananchi.

Miongoni wa Vitengo na idara zilitopewa saa 24 kuwasilisha taarifa kwake ni pamoja na kitengo cha Biashara,kitengo cha afya ,usafi na mazingira,Ukusanyaji mapato ,Elimu ,pamoja na Kitendo cha ustawi wa jamii.

Mkuu wa wilaya ya Ilala raymond Mushi akizungumza mara ya kutolewa kwa agizo hilo amesema kinafuata ni utekelezaji wa maagizo hayo mara moja

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE