March 16, 2016

                        

Aliyekua kiungo wa Arsenal, Emmanuel Petit ameungana na mashabiki waliochoshwa na utawala wa meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger, kwa kumtaka akae pembeni na kuwapisha wengine.

Petit, ambaye aliwahi kutwaa ubingwa wa ligi ya nchini England (Premier League) pamoja na kombe la chama cha soka nchini humo (FA Cup) mara mbili chini ya Wenger, amekubaliana na msukumo ambao umekua ukitolewa na mashabiki kwa kumtaka mzee huyo wa kufaransa kuondoka.

                      

Amesema imekua ni vigumu kuwamini kama Wenger anaweza kubadilisha muelekeo wa mafanikio kwenye klabu hiyo kwa sasa, na kwake anaona ni wakati mzuri kwa meneja huyo aliyedai anamuheshimu kumpisha mtu mwingine ili akalie kiti chake.

Petit, ambaye kwa sasa anafanya shughuli za uchambuzi wa soka katika kituo cha televisheni cha Canal+ cha nchini kwao Ufaransa, amesisiza kuwa, hakuna njia mbadala kwa Wenger kutwaa ubingwa wa England ama ule wa barani Ulaya kwa sasa kutokana na ushindani kuendelea kukua siku hadi siku, na wakati mwingine huamini mbinu zake zimepitwa na kasi ya michuano hiyo.

Amedai kwamba kushindwa kutetea ubingwa wa kombe la FA baada ya kutolewa na Watford mwishoni mwa juma lililopita, ni ishara tosha ambayo inamuaminisha yeye kama mchezaji aliyewahi kucheza chini ya urtawala wa Wenger, hakuna zuri lijalo kwa Arsenal zaidi ya kuendelea kupata aibu ya kumaliza msimu huu bila chochote mkononi.

Mtazomo huo wa Petit, unakuwa tofauti ule wa mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Ian Wright, ambaye aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari akisema kwamba, Wenger anapaswa kuachwa na kufanya kazi yake klabuni hapo kutokana na kuwa ufanisi mkubwa.

Wright, alikwenda mbali zaidi kwa kuwataka mashabiki wanaompinga babu huyo, kuacha kabisa kufanya hivyo, kutokana na makubwa aliyoifanyia klabu hiyo hadi kufikia hatua ya kumiliki uwanja mkubwa kama wa Emirates uliopo kaskazini mwa jijini London.

Purukushani za mashabiki kumtaka Wenger aondoke ziliibuka kufuatia matokeo mabaya yanayowaandama kwa sasa, huku wengine wakichukizwa na mazuri yanayoonekana kwa Leicester City, ambayo wanaamini yalipaswa kuwa upande wa The Gunners.

Leicester City, inaendelea kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa nchini England kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo, huku ikiwa imeiacha Arsenal kwa tofauti ya point 11, kwenye msimamo wa ligi.

Related Posts:

  • Polisi jela kwa kumuua mwanaharakati    Polisi wawili nchini Rwanda, wamefungwa miaka 20 jela kwa kumuua mwanaharakati wa kupinga ufisadi, aliyekuwa anachunguza kashfa ya ulanguzi wa madini mpakani. Gustave Makonene, aliyekuwa anafanya kazi na sh… Read More
  • New Audio- Mperampera - Mash J ft Stamina Baada ya kufanya poa sana na wimbo wake wa Rimex ya John iliyoimbwa na yemmy Alade wa Nigeria na yeye kuipa jina la Penny, mwanamuziki toka mkoani Morogoro Mash J, safari hii imekuja tena na wimbo wake mpera mpera alio… Read More
  • Wafugaji wafunga minada ya mifugo Morogoro    Wafugaji jamii ya wamasai na wabarabaigi mkoani Morogoro wamefunga minada yote ya kuuza mifugo mkoani Morogoro kwa muda usiojulikana wakilalamikia serikali kushindwa kukomesha vitendo vya uon… Read More
  • UKAWA yatangaza kususia Kura ya Maoni   Vyama vya Siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi nchini Tanzania (UKAWA) leo vimetangaza rasmi kuwa vitasusia kushiriki kura ya maoni, kwa ajili ya kupitisha Katiba mpya April 30, 2015 Vyama vya Sias… Read More
  • UN: Ugaidi hauna mfungamano na dini maalumu    Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa, ugaidi haufungamani na dini au madhehebu fulani na kusisitiza kwamba viongozi wote wa dini ulimwenguni wanalaani na wanapinga kwa nguvu zao zote vit… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE