March 02, 2016


 

Kundi la muziki la nchini Kenya lililoshinda tuzo mbalimbali,  Sauti Sol, limeachia wimbo maalum wa kitaifa kwaajili ya kusindikiza staftahi (kifungua kinywa) kwa ushirikiano na kampuni ya Unilever Kenya. HIGHER-HAIYA! Ni wimbo halisi wa kuchezeka wenye ujumbe mzito wa kutuhamasisha sote. Wimbo umetumbuizwa na Sauti Sol na umeandikwa na wao wenyewe wakishirikiana na Tim Rimbui na kurekodiwa/kutayarishwa na Tim ‘Timwork’ Rimbui wa Ennovatormusic.

“Wimbo ni mzuri na ni ukumbusho mwingine kwamba mwanzo mzuri ni kiashirio cha kwanza cha mwisho wake. Ni muhimu kwamba staftahi inatayarishwa kwaajili ya washindi; kwanza tunakuwa hivi tulivyo kwa kile tulichofunguliwa kinywa asubuhi na siku njema huanza asubuhi,” yamesema maelezo ya Sauti Sol.

Upate wimbo HIGHER-HAIYA!  na artwork yake kwenye ambatanisho la email hii. Kuwa huru kusambaza uwezavyo kwenye mitandao unayoitumia.



Kwa maelezo zaidi: Fuata kwenye Twitter @BlueBandKenya #GoodBreakfastChallenge

MAELEZO MUHIMU
 Februari 2016, Sauti Sol walizindua santuri yao ya tatu: Live and Die in Afrika jijini Nairobi kama sehemu ya ziara yao ya kitaifa ya mwaka 2016 Live and Die in Afrika.  Live and Die in Afrika ilijumuishwa kwenye nyimbo 10 bora za BBC Africa kwa mwaka 2015 na albamu 15 bora za Okayafrica kwa mwaka 2015.

Walitajwa pia kwenye orodha ya Billboard Africa kama kundi lenye mustakabali mkubwa zaidi (Most Promising Music Group). Walitajwa  kwenye gazeti la The Standard kwenye orodha ya mwaka 2016 ya ‘Agenda Setters’ na pia kuwekwa kwenye jarida la DRUM la Afrika Mashariki kwenye orodha ya mwaka 2015 ya Movers and Shakers.

 Mwaka 2015, Sauti Sol walitengeneza vichwa vya habari duniani baada ya kutumbuiza na kucheza na marais, Barack Obama wa Marekani na Uhuru Kenyatta wa Kenya kwenye chakula cha jioni katika ikulu ya Nairobi. Kwa sasa ni kundi pekee ambalo picha yake imetundikwa kwenye ikulu ya White House. Washindi hao wa MTV Europe Awards (EMA) 2014 pia walishinda tuzo ya kundi bora la muziki Afrika Mashariki kwenye tuzo za Bingwa.

Tuzo zingine walizonyakua mwaka 2015 ni pamoja na wimbo wao ‘Sura Yako’ kuwa wimbo bora wa Afrika Mashariki kwenye tuzo za Kilimanjaro (Tanzania), kundi ambalo nyimbo zake zimepakuliwa zaidi kwenye tuzo za Mdundo na video bora ya Kenya kwa wimbo ‘Sura Yako’ kwenye tuzo za  Bingwa (Kenya) na kundi bora barani Afrika kwenye tuzo za AFRIMMA (Marekani) na tuzo za AFRIMA (Nigeria).

Download hapa

Related Posts:

  • NEW AUDIO/ BIO ft MR BLUE - NISEME  Kama unaikumbuka analamika, Bibi, kaniulizia na baadhi ngoma toka kwakE. Anaitwa BIO hapa kamshirikisha MR:BLUE mzigo unaitwa Niseme. SKILIZA KISHA WAWEZA KU SHARE … Read More
  • MAAJABU YA NAY WA MITEGO, AJIPA ZAWADI YA GARI Jana ilikuwa ni Siku ya Kuzaliwa kwa Mwanamuziki Ney wa Mitego na aliamua kufanya sherehe kwa mara ya kwanza kusherehekea siku hiyo kwa vile huu ndio mwaka wake wa kwanza kuwa na mafanikio katika muziki , Ney alian… Read More
  • RAY C AMTAHADHARISHA HADIJA KOPA Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C amefunguka kwa kudai kuwa ujio wake mpya kwenye muziki atakuja pia na nyimbo za taarab, huku akimtaka Khadija Kopa ajiandae. Akizungumza na Sporah Show hivi karibuni, R… Read More
  • MUNTALA TALA VENCHA, HAPPY BIRTHDAY 2 U MY BROTHER    Muntala Tala v, tala talent, tala presdent, Tala Vencha Rais wa Msasani, ni mmoja ya wadau wa media niliotokea kuwakubali sana , kutokana na tabia yake ya kujali kila aina ya mtu. Jamaa tumekuwa tukishauliana … Read More
  • MUME WA FLORA MBASHA ALIA NA MCHUNGAJI GWAJIMA Na Makongoro Going’ MUME wa mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha anayedaiwa kumbaka binti wa miaka 17 (jina lipo), Emmanuel Mbasha ameibuka mzimamzima na kumtaka Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE