Lile shindano la kumsaka mrembo Miss Tanzania limerudi rasmi na linatarajiwa kuzinduliwa Jumamosi March 19 2016 Dar es salaam.
Akizungumza na Ayo TV Mkurugenzi wa Lino Agency ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, Hashimu Lundenga amesema msimu wa mashindano ya urembo ya miss Tanzania kwa mwaka 2016 utazinduliwa katika Hotel ya Ramada resort iliyopo eneo la Kunduchi jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Moses Nnauye, uzinduzi huo utanogeshwa na Linah Sanga pamoja na msanii wa ngoma za asili Wanne Star. Baada
ya uzinduzi huo Dar es salaam, utahamia mkoani Arusha, na baadae kuanza
kwa mashindano ya urembo katika ngazi za vituo, Wilaya, Mikoa na Kanda.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment