Mamlaka
ya Udhibiti na Usimamizi Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA),
Mkoa wa Kilimanjaro kuwafikisha mahakamani madereva wote na makondakta
wanaowatoza abiria nauli kubwa tofauti na zilizopangwa na ofisi hiyo.
Hayo
yamesemwa leo na Kaimu Afisa Mfawidhi Bw.Tadei Mwita alipokuwa akijibu
kero ya mkazi wa mkoa huo kwa njia ya simu iliyotolewa na Gazeti la
Mwananchi Machi 04, mwaka huu,iliyozungumzia daladala zinazofanya
safari zake kati ya Moshi Mjini – Himo kuwatoza nauli ya shillingi 1000
abiria wanaoshuka maeneo ya Kiboriloni, Sango Pumuani na Kawawa road
tofauti na nauli iliyopangwa na SUMATRA katika vituo hivyo.
“Kuanzia
wiki ijayo wadau wote watakao kuja kuomba leseni kwa ajili ya
usafirishaji wa abiria ndani ya mkoa huu watahitajika kuonyesha nauli
watakazo toza abiria katika vituo vya katikati kabla ya kufika kituo cha
mwisho cha safari zao,” alisema Bw.Mwita.
Bw.Mwita
alisema hivi sasa SUMATRA Mkoa wa Kilimanjaro imeanzisha utaratibu wa
kuwataka wadau wote wanaotarajia kuanza kutoa huduma za usafiri wa
daladala mkoani hapo kuonyesha nauli watakazo toza katika vituo vya
katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho.
Hata hivyo
Afisa huyo aliwashauri wakazi wa maeneo kama kiboriloni kwa sasa
kupanda daladala za Kiboriloni kwa kuwa zipo nyingi ili kuepuka usumbufu
unaojitokeza.
Na Anitha Jonas – MAELEZO
0 MAONI YAKO:
Post a Comment