March 21, 2016



Mabalozi na wawakilishi wa nchi za Ubelgiji, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Hispania, Sweden, Switzerland, Uingereza na Marekani hivi leo wametoa tamko kuhusu uchaguzi wa marudio uliofanyika Zanzibar tarehe 20 Machi 2016:
 
“Tumesikitishwa na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wa kuendesha marudio ya uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, bila kuwepo makubaliano ya pamoja baina ya pande kinzani na ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa visiwani humo uliotokana na majadilino baina ya pande husika. 
 
“Ili uwe wa kuaminika na kukubalika ni lazima mchakato wa uchaguzi uwe jumuishi na unaowakilisha kwa dhati matakwa ya watu.
 
“Tunarejea wito wetu kwa Serikali ya Tanzania kuonyesha na kuchukua uongozi katika suala la Zanzibar na kujielekeza katika kupatikana kwa ufumbuzi wa mgogoro huu kwa kupitia mazungumzo baina ya pande husika kwa lengo la kudumisha amani na umoja katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
“Kwa mara nyingine tunawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa utulivu na ustahimilivu waliouonyesha katika kipindi chote cha mchakato huu na kuvitaka vyama vyote na wafuasi wao kuanzisha tena mchakato wa maridhiano ya kitaifa ili kupata ufumbuzi jumuishi, endelevu na wa amani.”

Related Posts:

  • Kutoka kwa Thierry Henry juu ya fainali ya leo UEFA 2015 Swali: Fainali ya UEFA itakuwa historia kubwa kati ya Barcelona au Jeventus. Wewe umewahi kufanikiwa mwaka 2009, unaweza kusema chochote juu ya usiku wa fainali ya UEFA? TH: Ni ngumu sana kufanikiw… Read More
  • Mbiyo za Urais ndani ya CCM, Mwigulu Nchemba achukua fomu leo      Mbio za kumpata mlithi wa kiti cha urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, zinazidi kushika kasi ndani ya chama cha mapinduzi-CCM baada ya wanachama kuzidi kuongezeka katika harakati za kumpata mgombe… Read More
  • Kituo cha tembo yatima chafunguliwa   Srikali ya Tanzania imeanzisha kituo cha kwanza cha tembo yatima mjini Arusha. Kituo hicho kinatarajiwa kuhifadhi watoto wa tembo waliopoteza wazazi wao kutokana na vitendo vya ujangili au sababu nyengine. Hatua … Read More
  • Mwasiti amshtua Babu Tale Ukimya wa msanii wa Bongo Fleva,Mwasiti Almas kwenye muziki umemshtua meneja wa msanii Diamond,Babu Tale. Babu Tale alimzungumzia msanii huyo hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano kwenye kipindi cha XXL ambapo a… Read More
  • Waziri:Mbeki ndiye aliyetoa fedha kwa FIFA    Thabo Mbeki Waziri wa michezo wa Afrika Kusini , Fikile Mbalula, sasa anasema rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki ndie aliyeruhusu ulipwaji wa fedha ,dola milioni 10 kwa FIFA , hela ambayo sasa i… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE