March 22, 2016

                         

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi, kufuatia kifo cha ghafla cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, Kilichotokea jana jioni tarehe 21 Machi, 2016.

Bi. Sara Dumba aliugua ghafla kuanzia jana mchana na baadaye kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Njombe (Kibena), ambako wakati akipatiwa matibabu alifariki dunia majira ya saa moja za jioni.

Katika salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kushitushwa na kifo cha ghafla cha Bi. Sara Dumba, ambaye amesema alimfahamu kwa uchapakazi wake, uaminifu na uadilifu katika utumishi wa umma na katika uongozi."Nimeshitushwa sana na kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, kwa mara nyingine Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye mchango wake ulikuwa bado unahitajika" amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amebainisha kuwa Marehemu Sara dumba atakumbukwa kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuhimiza maendeleo ya wananchi, hususani katika kilimo na ufugaji, kuhimiza nidhamu ya utumishi serikalini na kuwatetea wananchi wa hali ya chini wakati wote wa majukumu yake ya ukuu wa wilaya.

Rais Magufuli amesema anaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu mkubwa, katika kipindi hiki kigumu na pia amewataka wote kuwa na subira na uvumilivu.

Amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

22 Machi, 2016

Related Posts:

  • lowassa aiteka Tarime Vijana wa Mjini Tarime wakiongoza mapokezi ya Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, alipowasili mjini Tarime kwa Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 10, 2015.… Read More
  • Lowassa afunika Karatu Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani M… Read More
  • Kauli ya mgombea Urais kwa tiketi ya TLP, baada ya Mrema kumuombea kura Magufuri Mgombea urais kupitia chama cha TLP Macmillan Lyimo amesema anaunga mkono kauli ya mwenyekiti wake wa chama Mh. Augustine Mrema ya ‘kumpigia debe’ mgombea wa chama cha mapinduzi CCM, Dk John Magufuli, kwa madai kuwa … Read More
  • Slaa amfagilia Magufuli, aisifu ACT kupambana na ufisadi Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema anamkubali kwa asilimia 90 mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli akisema anafaa kwa nafasi hiyo kwa kuwa ni jasiri na ana uwezo wa kup… Read More
  • New Audio| King Kapita_ Vizabizabina| Download hapa Mwana muziki mwenye kipaji cha kukidhi haja toka nchini Tanzania King Kapita, amekuletea tena ngoma yake mpya kabisa aliyomshirikisha Cannibal Shaitta toka nchini Kenya wimbo unaitwa vizabizabina, wimbo ambao umefany… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE