March 22, 2016

                             

Kwenye ukurasa wake wa facebook Zitto Kabwe ameandika ujumbe kutoa taarifa hiyo, na kusema kuwa pia ameamua kufanya hivyo ili kupisha uchunguzi kufanyika, na pia memuandikia barua spika wa bunge ili uchunguzi huo ufanyike kwa haraka.

"Kuna tuhuma za rushwa dhidi ya Kamati mbalimbali za Bunge ikiwemo kamati ninayohudumu. Nimemwandikia Spika Kuomba Uchunguzi juu Ya tuhuma hizo na kwamba achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayekutwa kuhusika na vitendo vya rushwa, nimejiuzulu Ujumbe wa Kamati ili Kutoa Nafasi Ya Uchunguzi Husika", alioandika Zitto Kabwe.

Mapema mwaka huu wabunge waliteuliwa kuhudumu kwenye kamati mbali mbali, na Zitto Kabwe alipangwa kwenye kamati ya Huduma na maendeleo ya jamii, ampapo awali alikuwa akihudumu kwenye kamati ya hesabu za serikali. (PAC)

                     

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE